Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Noble asubiri mbili Fountain Gate

NOBLE Pict

Muktasari:

  • Noble aliondolewa kikosini Aprili 21, mwaka huu, baada ya timu hiyo kupoteza kwa mabao 4-0 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo Babati mkoani Manyara.

HATIMA ya kipa namba moja wa timu ya Fountain Gate, Mnigeria John Noble itajulikana baada ya msimu wa Ligi Kuu Bara kumalizika iwapo atasalia au ataondoka ndani ya kikosi hicho.

Fountain Gate inatarajia kumalizia mechi mbili dhidi ya Azam FC na Coastal Union, kisha atamalizana uongozi wa kikosi hicho.

Noble aliondolewa kikosini Aprili 21, mwaka huu, baada ya timu hiyo kupoteza kwa mabao 4-0 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo Babati mkoani Manyara.

Katika mchezo huo kipa huyo alidaiwa kufanya makosa ya kizembe ambayo yaliigharimu timu yake kipindi cha kwanza baada ya kuruhusu mabao mawili ambayo uongozi wa timu hiyo uliyatafsiri kama uzembe, huku aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Robert Matano akisema Noble 'alipeana', akimaanisha kutoa zawadi. Matano kwa sasa hayupo Fountain Gate.

Akizungumzia suala hilo kwa Mwanaspoti, mratibu wa timu hiyo, Wendo Makau alisema wana mawasiliano mazuri na kipa huyo licha ya kwamba hayupo kambini Arusha kwa maandalizi ya mechi za mwisho za ligi dhidi ya Coastal Union na Azam.

Alisema waliamua kumuondoa Noble na kumpa likizo ya muda kwa ajili ya usalama wake kwa madai kwamba kuna wachezaji wenzake walitishia kumpiga wakihisi alifanya makosa ya makusudi kuiumiza timu.

"Ile mechi tulikuwa tunaitaka hivyo wakati wa mapumziko ya kipindi cha kwanza kulitokea vurugu kubwa sana wachezaji wenzake walitaka kumpiga. Hata baada ya kumalizika mchezo pia kule kambini wachezaji walitaka kumpiga," alisema Makau.

"Sasa kwa ajili ya usalama wake tukaona ni vyema kumuondoa ndani ya kikosi ili akapumzike kwanza halafu baadaye ndio atarejea."

Aliongeza kuwa hatima ya kipa huyo ambaye alitamba msimu uliopita katika Ligi Kuu Bara akiwa Tabora United itaamuliwa baada ya msimu kumalizika ambapo uongozi utatoa uamuzi wa kuendelea naye au kumuacha akatafute changamoto pengine.

Makau aliongeza kuwa kwa sasa nguvu kubwa wanaielekeza kwenye mechi mbili za mwisho zilizosalia ambazo ni muhimu kushinda na kumaliza nafasi za juu kwenye msimamo kisha watamuita Noble mezani kumalizana.

Itakumbukwa kwamba, baada ya kipa huyo kusimamishwa na uongozi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Manyara ilianzisha uchunguzi dhidi yake baada ya kusikia mitaani kuwapo kwa tuhuma za rushwa, ambapo bosi wa Takururu mkoani humo, Bahati Haule alidai licha ya kutopata malalamiko lakini waliamua kuchunguza madai hayo.