Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga vs JKT mechi ya kibingwa

Muktasari:

  • Yanga ambao ndio mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wanakutana na JKT ambao nao waliibuka mabingwa wa Ligi ya Championship msimu uliopita timu zote zikicheza mchezo wa pili wa ligi msimu huu na kushinda.

YAMESALIA masaa machache kabla Yanga kushuka uwanjani kupambana na JKT Tanzania mchezo ambao utakuwa na sura ya ushindani wa kibingwa kwa timu zote mbili.

Yanga ambao ndio mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wanakutana na JKT ambao nao waliibuka mabingwa wa Ligi ya Championship msimu uliopita timu zote zikicheza mchezo wa pili wa ligi msimu huu na kushinda.

Ubingwa huo wa Yanga msimu uliopita waliuchukua baada ya michezo 30 wakishinda mechi 25 sare 3 wakipoteza 2 wakikusanya jumla ya alama 78, wanakutana na JKT ambayo kwenye mechi zake 28 za msimu uliopita walishinda 20 wakitoa sare 3 na kupoteza 5 wakijikusanyia alama 63 kwenye ubingwa wao.

JKT iliianza ligi kwa kuichapa Namungo ugenini kwa bao 1-0 huku Yanga nao wakianza kwa kishindo kwa ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya KMC ukiwa ndio ushindi mkubwa mpaka sasa tangu ligi ianze msimu huu.

Timu zote mbili zilitoa wafungaji bora kwa msimu uliopita ambapo JKT walibeba tuzo hiyo kupitia mshambuliaji wao Edward Songo aliyepachika jumla ya mabao 18 huku Yanga wao wakibeba tuzo hiyo kupitia aliyekuwa mshambuliaji wao Fiston Mayele aliyepachika mabao 17 akifungana na Said Ntibazonkiza 'Saido' wa Simba

Songo atakuwepo leo uwanjani kupambana na ukuta wa Yanga ambao tangu Ligi ianze haujaruhusu bao lolote msimu huu huku mshambuliaji huyo akitafuta bao lake la kwanza.

Mechi hii itakayopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi inakuwa mechi ya 7 kwa timu zote mbili ambapo JKT watakuwa katika maswali mazito wakitafuta ushindi wa kwanza dhidi ya Yanga kufuatia kuwahi kukutana mara 6 huku Yanga ikishinda michezo 5 wakitoa sare mechi moja.