Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aziz KI ataja mambo mawili mazito Yanga

Muktasari:

  • Nyota huyo ameondoka Yanga akiacha rekodi nzuri ya kushinda mataji tisa katika misimu mitatu aliyocheza huku akibainisha kwamba, amekiacha kikosi hicho akiamini hakitatetereka kutokana na nyota waliopo lakini pia amepanga kuwaaga rasmi mashabiki wa timu hiyo.

STEPHANE Aziz KI kwa sasa yupo nchini kwao Burkina Faso ambako ameenda kusalimia nyumbani kwao kabla ya kwenda Morocco kuanza majukumu rasmi ya kuitumikia Wydad Casablanca, lakini huku nyuma ametoa kauli iliyobeba mambo mawili makubwa.

Nyota huyo ameondoka Yanga akiacha rekodi nzuri ya kushinda mataji tisa katika misimu mitatu aliyocheza huku akibainisha kwamba, amekiacha kikosi hicho akiamini hakitatetereka kutokana na nyota waliopo lakini pia amepanga kuwaaga rasmi mashabiki wa timu hiyo.

Aziz KI ambaye ameitumikia Yanga kwa misimu mitatu, ameuzwa kwenda Wydad inayojiandaa kushiriki michuano ya Kombe la Dunia la Klabu itakayofanyika kuanzia Juni 14 hadi Julai 13, 2025.

Akizungumza na Mwanaspoti akiwa kwao Burkina Faso, Aziz KI alisema kabla ya kwenda Morocco ameenda kwanza nyumbani kusalimia.

Alisema ameondoka kwa hatua ya kimaendeleo na atawaaga rasmi mashabiki wa timu hiyo siku chache zijazo, huku akiamini kuondoka kwake hakuwezi kukiathiri chochote kikosi cha Yanga.

“Yanga bado iko salama na itaendelea kuwa hivyo kutokana na ubora wa kikosi nilichokiacha, lakini pia viongozi bora waliopo ndani ya klabu hiyo.

“Hesabu za viongozi wa timu hiyo pamoja na wachezaji niliowaacha naona kabisa nitaendelea kufurahia mafanikio ya kikosi hicho hata huku ninakokwenda,” alisema na kuongeza:

“Nimerudi kwanza nyumbani kuonana na familia na baada ya hapo nitasema wapi ninakwenda mara baada ya kumaliza kila kitu lakini nitatumia muda wangu kuwaaga rasmi Yanga.”

Wachezaji waliobaki eneo la ushambuliaji ambao namba zao zinaonekana kuwa nzuri ndani ya kikosi cha Yanga ni Pacome Zouzoua aliyefunga mabao tisa na asisti tisa, Prince Dube (mabao 13, asisti 8), Maxi Nzengeli (mabao 5, asisti 9) na Clement Mzize (mabao 13, asisti 3) ambaye naye inaelezwa atauzwa mwisho wa msimu huu.

Aziz ameondoka Yanga msimu huu akiwa na rekodi ya kufunga mabao tisa na asisti saba katika Ligi Kuu Bara huku msimu uliopita akiwa mfungaji bora wa ligi hiyo alipofunga mabao 21. Mechi ya mwisho kuichezea Yanga msimu huu ilikuwa Juni 18, 2025 dhidi ya JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, ikiwa ni nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA), Yanga ikishinda 2-0 na kufuzu fainali.

Kwa sasa Yanga imebakiza mechi tatu za Ligi kuhitimisha msimu ambazo ni dhidi ya Simba (Juni 15), Tanzania Prisons (Juni 18) na Dodoma Jiji (Juni 22).

Hata hivyo, mpango wa Aziz KI kuwaaga mashabiki wa Yanga unaweza kuwa wa njia mbili, kuutmia akaunti zake za mitandao ya kijamia kuandika ujumbe maalum kwa au kurudi mara moja kuaga rasmi kabla ya kuanza maisha mapya Wydad.

Katika ishu ya kurudi kuaga, hivi sasa inaonekana kuwa ngumu kwani Aziz KI amejumuishwa kwenye kikosi cha Burkina Faso kitakachocheza mechi mbili zilizopo kwenye Kalenda ya FIFA, dhidi ya Tunisia (Juni 2) na Zimbabwe (Juni (6). Kabla ya hapo, Mei 27 mwaka huu kikosi cha Wydad kitacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Sevilla ikiwa ni maandalizi ya Kombe la Dunia la Klabu.

Baada ya ratiba hizo kukamilika, wakati Yanga ikiwa na mchezo dhidi ya Simba Juni 15, Aziz KI atakuwa Marekani akiwa na kikosi cha Wydad ambacho kitacheza mechi ya kwanza ya michuano hiyo Juni 18 dhidi ya Manchester City, siku ambayo Yanga pia itacheza mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Kisha Juni 22 siku ambayo Ligi Kuu Bara itafikia tamati huku Yanga ikiwa mwenyeji wa Dodoma Jiji, Aziz KI chama lake la Wydad litaikabili Juventus kabla ya Juni 26 kumaliza makundi dhidi ya Al Ain.