Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hesabu za Tabora United zipo kwa kipa Mghana

TABORA Pict

Muktasari:

  • Taarifa kutoka katika timu hiyo ya 'Nyuki wa Tabora', zinaeleza mabosi wa kikosi hicho wanampigia hesabu kipa huyo raia wa Ghana, kwa sababu mkataba alionao na Asante Kotoko unafikia tamati Juni 30, 2025 na hakuna mazungumzo ya kuongeza mpya.

MABOSI wa Tabora United wameanza harakati za kukisuka upya kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao ili kuongeza ushindani katika michuano mbalimbali na wanampigia hesabu kipa, Fredrick Asare anayeichezea Asante Kotoko ya Ghana.

Taarifa kutoka katika timu hiyo ya 'Nyuki wa Tabora', zinaeleza mabosi wa kikosi hicho wanampigia hesabu kipa huyo raia wa Ghana, kwa sababu mkataba alionao na Asante Kotoko unafikia tamati Juni 30, 2025 na hakuna mazungumzo ya kuongeza mpya.

"Mazungumzo yapo hatua nzuri kwa sababu kinachofanyika ni kukubaliana masilahi binafsi tu, ni kipa mzuri anayecheza soka la kisasa ambaye tunaamini ataongeza ushindani na makipa wenzake waliopo katika kikosi chetu," kilisema chanzo chetu.

Akizungumza na Mwanaspoti kuhusu usajili wa kipa huyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tabora United, Charles Obiny alisema ni mapema kuzungumzia hilo kwa sasa, ingawa baada ya kumaliza msimu jana, ndipo watakaa na kufanyia tathimini ya jumla.

"Bado mchakato wa usajili ni wa ndani kwa ndani kwa sababu tunahitaji kufanya tathimini ya kina kwa kushirikiana pia na benchi letu la ufundi, lengo ni kujua ni maeneo gani muhimu ya kuyaboresha mapema kabla ya msimu ujao," alisema Obiny.

Asare aliyezaliwa Mei 28, 1999, ni miongoni mwa makipa wanaotajwa bora kwao Ghana, huku ikielezwa anavutiwa na soka la Tanzania kwa kiasi kikubwa, jambo linalomfanya kushindwa kufikia makubaliano ya mkataba mpya na mabosi wa Asante Kotoko.

Kipa huyo alijiunga na Asante Kotoko Agosti 2, 2022, akitokea Accra Lions FC ya kwao Ghana na mkataba wake unaisha Juni 30, 2025, jambo linalowafanya mabosi wa Tabora kumhitaji ili kuongeza ushindani kwa mwenzake, Jean-Noel Amonome.

Jean-Noel Amonome raia wa Gabon amekuwa panga pangua katika kikosi cha Tabora tangu ajiunge nacho Januari 2025, akitokea AS Arta/Solar7 ya Djibouti, hivyo endapo dili la Asare litakamilika ataenda kuongeza ushindani kikosini humo msimu ujao.