Yanga, Dodoma ngoma ngumu

Kipindi cha kwanza, mchezo kati ya Dodoma Jiji na Yanga kimemalizika kwa suluhu kwenye uwanja wa Jamhuri.
Timu zote zilishambuliana mara kadhaa lakini maahambulizi yao hayakuzaa bao lolote kwa kila upande.
Dodoma walianza kwa shuti la Anuary Jabir lililodakwa na Kipa Ramadhani Kabwili, kabla ya mashuti mengine ya Cleophas Mkandala na Mcha Khamis yaliyookolewa na Kabwili.
Upande wa Yanga, mashuti ya timu hiyo yaliyolenga lango, yalipigwa na Wazir Junior na Paul Godfrey, yaliyookolewa na kipa Hussein Dotto.
Umahiri wa kipa Dotto, uliwanyima pia Yanga mabao kufuatia kuokoa vema michomo ya Lamine Moro na Wazir Junior pamoja na Godfrey kabla ya kutengeneza kona.
Kiujumla timu zote zimeshambuliana kwa nyakati tofauti, jambo linalofanya kipindi cha pili kiwe cha kuamua.