Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

YALIYOJIRI MJENGONI: 'Ubaya Ubwela' ilivyomchanganya Dk Bashiru

BASHIRU Pict

Muktasari:

  • Yaani Balozi Dk Bashiru Kakurwa amesema misamiati ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso yote anaielewa isipokuwa huo ambao haupo kwenye kamusi yake.

Dk Bashiru kwani misamiati yote aliyoitoa Waziri unataka kutuambia unaijua isipokuwa hilo moja tu.

Yaani Balozi Dk Bashiru Kakurwa amesema misamiati ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso yote anaielewa isipokuwa huo ambao haupo kwenye kamusi yake.

"Mheshimiwa Spika, nimemuelewa Waziri kwa kila neno na maneno yake magumu na misamiati yote, isipokuwa neno moja la 'Ubaya Ubwela' ndilo ambalo sikulielewa," alisema Dk Bashiru.

Ulizo lake lilitokana na Hotuba ya Waziri wa Maji wakati wa maombi ya fedha kwa mwaka 2025/26 ambapo alipiga mabombastiki kama yote kwenye hotuba hiyo.

Hata hivyo, kabla ya kuhitimisha hotuba yake Waziri akasema anaipongeza sana Klabu ya Simba kwa kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika,  ndipo akasema "Huu ndio 'Ubaya Ubwela'.

Sasa Balozi hilo neno likawa gumu kwake kiasi cha kuanza kumchanganya, huenda ni kwa sababu ya misamiati mpya huo ambao umekubaliwa na vitabu vingine vyote hapa nchini.

Ngoja nimkumbushe mahali anapoweza kuupata msamiati huu, Dk Bashiru nenda Mtaa wa Msimbazi haya maneno ni ya kawaida mbona wala huhitaji kujiuliza sana.

Ahaa, kumbe wewe ni wa Jangwani, basi ndiyo maana hujui misamiati ya kisasa Baba inabidi uwe mpole sasa.