Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa idadi ya wapiga kura RT, viongozi wakimbilia kwa Prof Kabudi

RT Pict

Muktasari:

  • Mkutano Mkuu wa marekebisho ya Katiba ya RT ulifanyika Aprili 28 mwaka huu jijini Mwanza ambapo wajumbe walifanya maamuzi kwenye baadhi ya vipengele vya katiba hiyo.

Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) imeweka wazi inashindwa kutangaza tarehe ya Mkutano Mkuu wa Uchaguzi Mkuu kwa sababu kuna baadhi ya viongozi  hawakuridhika na maamuzi yaliyofanyika kwenye Mkutano Mkuu wa Katiba hivyo kuandika barua kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof Palamagamba Kabudi kupinga maamuzi ya mkutano huo.

Mkutano Mkuu wa marekebisho ya Katiba ya RT ilifanyika Februari 28 mwaka huu, jijini Mwanza ambapo wajumbe walifanya maamuzi katika baadhi ya vipengele vya katiba hiyo.

Ambapo baada ya hapo ilitarajiwa katiba kupitishwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ili kuruhusu mchakato wa uchaguzi kuanza, lakini hali imekuwa ni tofauti kwani hadi sasa haijapitishwa na msajili.

Kaimu Katibu Mkuu wa RT, Jackson Ndaweka ameiambia Mwanaspoti kwamba baada ya Mkutano Mkuu wa Mwanza kuna viongozi ambao hawakuridhika na maamuzi ambayo yalifanyika hasa katika baadhi ya vipengele vya katiba hiyo.

Iliyokuwa inasema wapiga kura kwenye maamuzi yoyote ya Mkutano Mkuu wawe ni wenyeviti wa mikoa lakini miongoni mwa vipengele ambavyo kamati ya utendaji iliidhinisha hili vipelekwe katika mkutano Mkuu kwa ajili ya marekebisho,  idadi ya wapiga kura yenyewe haikuguswa.

Hali iliyofanya mjadala wake kushindwa kufikia hitimisho kwa sababu haikuwa kwenye ajenda, hapo ndipo ikatokea shida kwa wajumbe ambao hakuridhika hivyo kuamua kuandika barua kwenda kwa Waziri na wasaidizi wake ambayo imepelekea usajili kusitishwa kwanza,ili kusubiri maelekezo kutoka kwa Waziri.

“Wiki mbili zilizopita viongozi tuliitwa na msajili tukakaa kikao ikatolewa maelekezo ya maeneo ambayo pamoja na yale  yaliyoidhinishwa na Mkutano Mkuu, lakini walikuwa wanaona kuna maeneo kwa masalahi ya maendeleo ya mchezo wa riadha yanahitaji kurekebishwa,” amesema Ndaweka.

Anaongeza baada ya hapo wakairekebisha ila kukawa tena na maeneo mengine ambayo yanasubiri maelekezo kutoka kwa Waziri, hivyo sasa inawafanya kushindwa kuitisha Mkutano wa Uchaguzi, kwani hawawezi hadi kupitishwa kwa marebisho ya katiba kwa msajili. 

“Tumewasiliana na msajili ametulekeza kukutana nae wiki ijayo kwa ajili ya mrejesho ya yale ambayo yalikuwa yamebakia hivyo tunatarajia baada ya kwenda kwake kila kitu kitakuwa sawa,” ameongeza.

Ndaweka amesema changamoto kubwa ambayo ipo kwa sasa kuna baadhi ya viongozi ambao bado wanataka itumike mfumo wa zamani wa upigaji kura badala ya ile ya sasa ambayo inafuata muongozo wa Shirikisho la Riadha la Dunia.

Muongozo huo ni unataka kila nchi mpiga kura anakuwa mmoja yaani Rais, hivyo kwa RT nayo mpiga kura anakuwa Mwenyekiti wa Mkoa.

“Huko nyuma kabla ya marekebisho ya mwaka 2020, kura ilikuwa inapigwa na watu watatu kutoka chama kimoja cha Mkoa, ambao ni mwenyekiti, katibu na mjumbe wa mkutano mkuu.”

“Lakini marekebisho ya mwaka 2020 kuja katiba mpya ikaondoa na kufuata mfumo wa Shirikisho la Riadha la Dunia, kwamba kura ipigwe na Mkoa ambapo mpigaji ni mwenyekiti, akikosekana Makamu au Katibu," amesema Ndaweka.

Ndaweka anaamini uwezekano wa uchaguzi huo kushindwa kufanyika ni mdogo sana na kuongeza matamanio ni kuona ikifanyika Juni mwaka huu.

“Kuna viongozi wetu wengine wana mitazamo tofuati wana fikiri kuwe na makatibu ambao nao watapiga kura kwa sababu zao,” amesema Ndaweka.