Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wenye mili mikubwa, watunisha misuli kukiwasha Desemba 3

Muktasari:

DESEMBA 3, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kutakuwa na mashindano mbalimbali ya watu wenye mili mikubwa (Boardgard) na wale watunisha misuli ambalo litaandaliwa na (Strongest Man Challeng in Tanzania).

DESEMBA 3, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kutakuwa na mashindano mbalimbali ya watu wenye mili mikubwa (Boardgard) na wale watunisha misuli ambalo litaandaliwa na (Strongest Man Challeng in Tanzania).

Meneja masoko wa Strongest Man Challeng in Tanzania, Fred Mwakisitu alisema shindano hilo linadhumini la kumtafuta mtu mwenye nguvu zaidi nchini awe mwanaume au mwanamke.

Mwakisitu alisema michazo ambayo itachezwa ni mtu mmoja kufunga kamba kwenye gari na kulivuta mwenyewe, kuamisha vitu vizito kutoka katika eneo moja kwenda lingine, kurusha tufe lenye uzito zaidi, kulala chini gari kupita juu yake pamoja na mengineyo.

Alisema ili kushiriki mchezo huo vigezo vyake vinatakiwa mshiriki awe na afya njema, watu wenye nguvu, mabaunsa, watunisha misuli, wanafunzi wa vyuo, wabeba mizigo mikubwa wale masokoni na mwananchi yoyote ambaye anajiamini anaweza kucheza.

"Katika shindano hili kutakuwa na hatua tatu tofauti tutaanza na ile ya awali ambayo uzito wa kitu kinachofanywa au kubebwa hakitakuwa mkubwa zaidi kama ule wa hatua ya tatu," alisema Mwakisitu na kuongeza;

"Yule ambaye ataweza kufanya mashindano yote hayo matatu kwa muda mchache ndio atakuwa mshindi wetu na atapata zawadi kubwa kulingana na kazi ambayo atakuwa ameifanya."

Mwenyekiti wa mabodigadi nchini, Faraji Robart alisema awali walikuwa hawana mashindano rasmi kutokana na miili yao ilivyo zaidi ya kufanya kazi ya ulinzi wa watu binafsi na maeneo mengine.

"Haya mashindano yanakwenda kutupa ajili nyingine kama vijana ambao wengi wao tupo mtaani na tunaomba Strongest Man Challeng in Tanzania wasiishie hapa waendelee mbele zaidi kwani tunaweza kupata wawakilishi wa nchi katika mashindano ya Olimpic," alisema Robart.