Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wastara huyoo anasepa

Muktasari:

  • Dk. Magufuli na mkewe, walimchangia Sh15 milioni huku nyingine zikitolewa na wadau mbalimbali na kumwezesha mwigizaji huyo kuwahi India kwa matibabu anayotakiwa kufanyiwa wiki ijayo.

MWIGIZAJI nyota wa filamu nchini, Wastara Juma, mchana huu anatarajiwa kupaa zake kwenda India kwa ajili ya kupata matibabu baada ya mchango wa Rais Dk. John Magufuli na mkewe Mama Janeth, sambamba na wadau wengine waliompiga tafu.

Dk. Magufuli na mkewe, walimchangia Sh15 milioni huku nyingine zikitolewa na wadau mbalimbali na kumwezesha mwigizaji huyo kuwahi India kwa matibabu anayotakiwa kufanyiwa wiki ijayo.

Akizungumza na Mwanaspoti jana Jumamosi, Kaka wa Wastara, Issa Juma, alisema tayari taratibu zote safari zimekamilika ambapo, anatarajiwa kupaa majira ya saa saba mchana na Shirika la Ndege la Ethiopia.

Katika safari hiyo, Juma alisema dada yake huyo atasindikizwa na ndugu wawili ambao, watakuwa wakimsaidia wakati akipatiwa matibabu hayo.

Wastara alichangiwa fedha hizo baada ya kuandika kwenye mtandao wa kijamii mapema mwezi uliopita, akiwalilia Watanzania wamchangie ili kwenda kwenye matababu yake kufuatia kuteswa na maumivu na huku hakuwa na fedha za kutosha kugharamia matibabu.

Ndipo wiki iliyopita Dk. Magufuli na mkewe waliguswa na kilio hicho cha Wastara na kumchangia Sh15milioni, kitendo kilichomfanya angalau kupumua na sasa anakwea pipa mchana huu kama masihara vile.