Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waliopoteza tiketi uhakika Kwa Mkapa

TIKETI Pict

Muktasari:

  • Akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa, N-Card wamejipanga kuhakikisha kuwa kila aliyekata tiketi basi ana nafasi ya kuingia uwanjani.

KIONGOZI wa N-Card Catherine Chami amewapa uhakika mashabiki waliopoteza tiketi zao ambazo walizikata kwa ajili ya mechi ya Dabi ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba iliyotakiwa kuchezwa Machi 8, 2025 bado wana nafasi ya kuingia uwanjani Benjamin Mkapa katika tarehe mpya iliyopangwa ya mechi hiyo Juni 25.

Akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa, N-Card wamejipanga kuhakikisha kuwa kila aliyekata tiketi basi ana nafasi ya kuingia uwanjani.

"Kwa wale ambao tiketi zilipotea basi wanaweza kufika katika ubalozi wa Ufaransa ili waweze kusaidiwa mapema kuepuka usumbufu siku ya dabi.

"Ila kwa upande wa wenye tiketi hawana shida kwani wataingia uwanjani kama kawaida kwa njia ya 'kuswap' kadi zao."

Ofisa Habari wa TPLB, Karim Boimanda alisema kuwa; "Bodi ya Ligi na timu mwenyeji zitaungana kuhakikisha kuwa mashabiki hawapati changamoto yoyote kwa wale waliokata tiketi."

"Mashabiki watakaofika siku hiyo watapata faida mbili ya kwanza kushuhudia dabi na pili kuiona fainali ya bingwa wa Ligi Kuu Bara."