Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Asaka rekodi ya kupanda Mlima Kilimanjaro akipiga danadana

DANADANA Pict

Muktasari:

  • Staa huyo wa dunia anayetikisa dunia, Emil Jylhanlahti, sasa amepewa majukumu mapya kuwa mkuu wa programu ya soka kwa watoto wa Norrby IF nchini Sweden.

WAKATI wengine hupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutembea kawaida, staa wa danadana kutoka Sweden, Emil Jylhänlahti, ameanza safari ya kuupanda mlima huo maarufu duniani huku akichezea mpira kwa danadana.

Staa huyo wa dunia anayetikisa dunia, Emil Jylhanlahti, sasa amepewa majukumu mapya kuwa mkuu wa programu ya soka kwa watoto wa Norrby IF nchini Sweden.

Nyota huyo ambaye pia ni mkuu wa programu ya soka kwa watoto wa Norrby IF nchini Sweden amewahi kushirikiana na mastaa wakubwa wa soka duniani, sasa anataka kutumia kipaji chake kuwasaidia watu wanaoishi kwenye mazingira magumu vijijini.

Emil ameanza safari yake leo Juni 23, 2025 kupitia lango la Marangu akiwa na lengo la kuweka rekodi ya aina yake duniani pia kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia watu wanaoishi kwenye mazingira magumu vijijini.

Akizungumza na Mwananchi kabla ya kuanza safari hiyo, Emil amesema, “Nataka kuonyesha kuwa mpira unaweza kuwa zaidi ya burudani, unaweza kuwa chombo cha kusaidia maisha ya wengine. Ndiyo maana nimeamua kupanda mlima huu kwa kucheza danadana ili kuhamasisha watu kusaidia walio na uhitaji.”

Kabla ya safari yake, Emil jana alitembelea maeneo mbalimbali ya Mji wa Moshi akionyesha ustadi wake wa kuchezea mpira kwa muda mrefu, jambo lililowavutia wakazi waliomshuhudia.

Safari hiyo ya Emil inatarajiwa kuchukua siku sita hadi kufika kileleni, ambapo amesema atapiga danadana tena kwenye kilele cha Uhuru (Uhuru Peak), ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha safari yake ya kihistoria.

Mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu zaidi barani Afrika, umekuwa kivutio kwa wageni wengi kutoka mataifa mbalimbali duniani wanaotafuta kuvunja rekodi au kutangaza ujumbe wa kijamii, ambapo hivi karibuni mwanajeshi kutoka Uingereza alipanda mlima huo akiwa amebeba friji.

Kwa mujibu wa TFS, zaidi ya wageni 50,000 hupanda Mlima Kilimanjaro kila mwaka, na wengi wao wamekuwa wakitumia mbinu tofauti kutangaza dhamira zao.