Wanariadha wa jeshi, Ambassador waibeba Tanzania Km 5

Muktasari:
Kwa upande wa wanaume walioshiriki kilomita 5 mwanariadha Ambroce Sadick wa Ambossador aliibuka mshindi akimaliza kwa kutumia dakika 14:14:56, akifuatiwa na Marco Silvester Monco wa Jkt 14:23:09, na mshindi wa tatu ni Daniel Sinda wa 'team Simbu' aliyetumia dakika14 :26:47.
BERTHA ISMAIL -ARUSHA Wanariadha kutoka klabu za jeshi na Ambassador kutoka Arusha wamefanikiwa kutwaa ushindi wa mbio za Ngorongoro Race kwa upande wa umbali wa kilomita 5 kwa wasichana na wavulana.
Kwa upande wa wasichana mwanariadha Cecilia Panga kutoka JWTz amefanikiwa kuibuka na ushindi baada ya kumaliza umbali wa km 5 akitumia dakika 16:37:29, akifuatiwa na Sara Hiiti wa Jkt aliyetumia dakika 17:08:66, huku nafasi ya tatu ikienda kwa Sara Ramadhani wa Arusha aliyetumia dakika 17:13:36.
Kwa upande wa wanaume walioshiriki kilomita 5 mwanariadha Ambroce Sadick wa Ambossador aliibuka mshindi akimaliza kwa kutumia dakika 14:14:56, akifuatiwa na Marco Silvester Monco wa Jkt 14:23:09, na mshindi wa tatu ni Daniel Sinda wa 'team Simbu' aliyetumia dakika14 :26:47.
Washindi hao wamefanikiwa kuvishwa medali na waziri wa mali asili na Utalii Hamis Kigwangala. Akizungumza na waandishi wa habari mshindi kwa upande wa wanawake Cecilia amesema kuwa ametumia hizo kwa ajili ya kujipima uwezo, nguvu na pumzi kwa ajili ya mbio ndefu za mashindano ya kimataifa.