Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wambura, Aveva wote chupuchupu Msimbazi

Wambura

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa kamati hiyo, Damas Ndumbaro alisema kuwa vitendo hivyo ni batili na mgombea yeyote atakayeendeleza vitendo kama hivyo kabla ya kufunguliwa rasmi kwa kampeni ataondolewa katika kinyany’anyiro hicho.

KAMATI ya uchaguzi ya Simba imetoa onyo kwa wagombea wote waliokwenda kuchukua na kurudisha fomu kwa kufanya vitendo vilivyohusishwa na kampeni ikiwemo kile cha Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali na mchezaji wa zamani wa Simba Athur Mwambeta kuwasifia Evance Aveva na Michael Wambura wakati wa kurejesha fomu.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Damas Ndumbaro alisema kuwa vitendo hivyo ni batili na mgombea yeyote atakayeendeleza vitendo kama hivyo kabla ya kufunguliwa rasmi kwa kampeni ataondolewa katika kinyany’anyiro hicho.

Mapema wiki iliyopita Dalali alimsindikiza mgombea Aveva kurejesha fomu ya kuwania Urais  na alipopewa nafasi ya kuzungumza chochote alianza kumpigia debe mgombea huyo kitu ambacho ni kinyume na taratibu za uchaguzi za Simba. Naye Mwambeta alijitokeza kumsindikiza Wambura na kufanya hivyohivyo.

“Kwa bahati mbaya hatukutoa maelekezo ya kutosha wakati zoezi linaanza ila tumesikitishwa na kuwapo kwa vitendo kama hivyo, napenda kuanza na adhabu ya chini kwenye kanuni zetu ya kuwapa onyo wagombea ila ukiukwaji huu wa kanuni ukiendelea tutawaondoa kabisa katika kinyang’anyiro.

“Kamati imepitisha majina ya waliochukua fomu baada ya kuhakiki kama waliweka viambata vyote vilivyohitajika kwenye fomu zao, zoezi linalofuata kwa sasa kupokea mapingamizi,” alisema Ndumbaro ambaye ni mwanasheria na kuongeza

“Mapingamizi hayo yatapokelewa kwa siku tatu kuanzia kesho (leo Jumanne) mpaka Alhamisi ya tarehe 22 na kamati itakutana tarehe 25 ya mwezi huu pamoja na walioweka na kuwekewa mapingamizi hayo ili kuyajadili.”

Majina ya wagombea yaliyotolewa na kamati ni kama ifuatavyo: Urais ni Andrew Tupa, Evance Aveva na Michael Wambura. Makamu ni Swedi Mkwabi, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, Bundala Kabulwa, Joseph Itang’are ‘Mzee Kinesi’, Emmanuel Mayage na Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’.

Wajumbe ni Selemani Dewji, Chano Hassan, Yasin Mwete, Ally Chaurembo, Abdulhamid Mshangama, Juma Pinto, Emmanuel Kazimoto, Damian Manembe, George Wakuganda, Said Pamba, Salim Seif, Ahmed Mlanzi, Alfed Elia, Saidi Kubenea, Hamis Mkoma, Ibrahim Masoud ‘Maestro’ na  Collin Frisch.

Wajumbe wengine ni Rodney Chiduo, Omary Omary, Idd Mkamballah, Said Tulliy, Juma Mussa, Hussein Simba, Ramson Rutiginga, Ally Suru, Maulid Abdallah na Iddy Kajuna. Wajumbe wanawake ni Amina Poyo, Asha Kigundula, Asha Muhaji na Jasmine Suddy.

Kwa upande mwingine klabu ya Simba imeifanyia marekebisho kamati yake ya uchaguzi kwa kupunguza wajumbe wawili. Wajumbe waliopunguzwa ni Juma Simba ‘Ghadafi’ na Kassim Dewji huku Salum Madenge akienguliwa ili kumpisha wakili Evodi Mmanda aliyechukua nafasi ya Makamu Mwenyekiti.