Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakongwe watikisika BDL

WAKONGWE Pict

Muktasari:

  • KIUT ilionyesha ubabe wake kwa kuichapa JKT kwa pointi 84-74, kisha kuifunga UDSM Outsiders kwa pointi 64-53 na kocha wa timu hiyo, Denisi Funganoti alisema mipango waliyojiwekea ya kufanya vizuri katika michuano hii ndiyo chachu ya ushindi.

KIUT na DB Oratory zimeendelea kuzitikisa timu kongwe zinazoshiriki Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) kutokana na kutokuzihofia na kuzitembezea vichapo.

KIUT ilionyesha ubabe wake kwa kuichapa JKT kwa pointi 84-74, kisha kuifunga UDSM Outsiders kwa pointi 64-53 na kocha wa timu hiyo, Denisi Funganoti alisema mipango waliyojiwekea ya kufanya vizuri katika michuano hii ndiyo chachu ya ushindi.

“Tulikuwa tunabezwa sana kutokana na uchanga wa KIUT, lakini tutapambana na timu yeyote tutakayocheza nayo,” alisema Funganoti.

Nyota wa timu hiyo, Adamu Michael alisema ushindi huo umechangiwa pia na marekebisho ya makosa waliyokuwa wanafanya katika michezo ya mwanzo.

“Kwa kweli zoezi la kurekebisha makosa lilifanikiwa, tulibadika na timu zote kwa sasa zimeanza kutuhofia,” alisema Michael.

Kwa upande wa DB Oratory iliifunga Srelio kwa pointi 76-72, kisha ikaifunga  Savio kwa pointi 75-60.

***

Noela, Juliana wachuana kwa asisti

WAKATI ushindani kwa timu za wanawake ukizidi kushika kasi katika Ligi ya Kikapu Dar es Salaam (WBDL), kwa upande wa asisti, Noela Uwendameno kutoka  Jeshi Stars anaongoza kwa kutoa 34.

Noela ambaye msimu uliopita aliichezea Vijana Queens, msimu huu ameonyesha kiwango kizuri akiwa na Jeshi Stars, huku Juliana Sambwe wa Tausi Royals anayecheza nafasi ya namba 1 (Pointi Guard) ni pili akiwa na asisti 31.

Wachezaji wengine ni Jesca Lenga (DB Troncatt0-28), Tumaini Ndossi (Tausi Royals-22) na Elina Sinamenga (Twalipo Queens-22)  

Kwa upande wa kunyakua mipira (Steal), Sambwe anaongoza kwa kufanya hivyo mara 14, akifuatiwa na Salma Sandali wa Vijana Queens (9).

Wachezaji wengine ni Elina Sinamengo wa Twalipo Queens (8), Mahewa Matema,  Tausi Royals (8) na Noela Uwendameno, Vijana Queens (8).

Steal ni neno linalotumika baada ya mchezaji kunyakua mpira kutoka kwa  mpinzani wake bila ya kumfanyia madhambi.

Katika ribaundi anayeongoza ni Taudencia Katumbi wa DB Lioness aliyedaka  mara 74, akifuatiwa na Jacklini Mgaiwa wa City Queens (57).

Wengine ni Marshallet Shimbweche wa Reel Dream (53), Anamary Cyplian wa Jeshi Stars (48) na Nadjima Manji wa Ukonga Queens (45).