Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waliomwaga wino Yanga, Simba wasibweteke

Mchezaji wa Yanga aliyesajiliwa kutoka Mgambo JKT, Malimi Busungu

Muktasari:

Kwa siku za karibuni tumesikia habari za Peter Mwalyanzi, Mohammed Abraham Mohammed, Samir Nuhu, Mohammed Faki waliosajiliwa Simba.

KASI ya usajili wa wachezaji kwa ajili ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2015/16 imeendelea kupamba moto huku klabu za Simba, Yanga na Azam zikichuana vikali.

Kwa siku za karibuni tumesikia habari za Peter Mwalyanzi, Mohammed Abraham Mohammed, Samir Nuhu, Mohammed Faki waliosajiliwa Simba.

Yanga nako si haba, tumesikia habari za klabu hiyo kukamilisha usajili wa mchezaji, Malimi Basungu aliyetanguliwa na kina, Benedictor Tinoco, Mwinyi Haji Mngwali na Deus Kaseke.

Kama ambavyo tumekuwa tukiwasikia mara kwa mara wachezaji katika Ligi Kuu England au Ulaya kwa ujumla kuwa kuna baadhi ya timu ambazo kila mchezaji anakuwa na shauku ya kutaka kuzichezea.

Kuna wengine ambao husema kwamba wamekuwa wakizipenda timu hizo tangu utotoni na kwamba moja ya ndoto zao wakati wanachipukia katika soka ni kuhakikisha wanapata nafasi ya kuichezea moja ya klabu hizo.

Mfano ni Memphis Depay, winga wa klabu ya PSV ya Uholanzi ambaye yuko katika hatua za mwisho kujiunga na klabu ya Manchester United lakini tayari amenukuliwa akisema kwamba ndoto yake ya tangu utotoni ilikuwa ni kuichezea timu hiyo.

Na kwa kuwa kwa hapa Tanzania klabu za Yanga na Simba ndizo kongwe, kubwa na zenye mashabiki wengi ni wazi wapo wachezaji wengi ambao wana shauku kubwa ya kuwa wachezaji wa timu hizo.

Katika mtazamo huo huo ni wazi kwamba hawa wachezaji ambao wamesajiliwa hivi karibuni wengi wao kama si wote watakuwa wametimiza ndoto zao katika soka.

Kwa sasa wanajisikia faraja kubwa baada ya kumwaga wino na hivyo kuwa wachezaji halali wa klabu za Simba na Yanga na kwamba wataonekana wakiwa na jezi za timu hiyo katika ligi na michezo mingineyo.

Ushauri wetu kwa wachezaji hao ni kuwa makini na kutokubali kubweteka na kujiona kama vile Simba na Yanga ndio kila kitu katika soka.

Kufanya hivyo itakuwa kosa kubwa kwani ipo mifano ya wachezaji wengi ambao wamecheza katika timu hizo kwa msimu mmoja tu tena msimu wenyewe wamecheza mechi zinazohesabika na wengine hawajacheza mechi hata moja.

Hili ni jambo ambalo wachezaji hawa ambao wanaingia Simba na Yanga kwa mara ya kwanza wanatakiwa kuliangalia kwa umakini na kulifanyia kazi.

Ni ukweli usiofichika kuwa kwa Tanzania mchezaji anapopata nafasi kusajiliwa Yanga au Simba anakuwa ameonyesha kitu fulani au amefanya kitu cha kipekee uwanjani na hiyo kuwa sababu ya kuwashawishi viongozi wa timu hizo kuanza harakati za kumsajili.

Sambamba na hilo pia kuna ukweli kwamba wachezaji hao hao baada ya kuonyesha hicho walichokionyesha hadi kupata nafasi ya kwenda Yanga au Simba hujikuta wakibweteka.

Hali hii ya kubweteka si nzuri hasa unapouzingatia ukweli kwamba Yanga na Simba pamoja na ukongwe wao lakini bado si klabu zenye maendeleo ya kutisha na zinazoweza kumlipa mchezaji fedha za maana.

Tungependa kuona wachezaji hawa wanafikiria maisha nje ya Yanga na Simba baada ya usajili wao kwa kufanya juhudi ili wasajiliwe na klabu nyingine kubwa za nje ya nchi na hilo litafanikiwa kama hawatabweteka kwa kuvaa jezi nyekundu na nyeupe au kijani na njano.