Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakaa benchi Simba wapewa muda

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salum Abdallah 'Try Again' amewapa mwezi mmoja na nusu mastaa wao kutumia kipindi hicho kujihakikishia nafasi ya kubaki kikosini.

Hayo ameyazungumza leo Novemba 14, 2023 wakati akihojiwa na Azam Tv, akizungumzia juu ya mpango wao wa usajili wakati wa dirisha dogo linalotarajiwa kufunguliwa Desemba mwaka huu ambapo amekiri kuwa wataachana na wachezaji wote ambao wameshindwa kuipambania timu.

"Tuna mwezi mmoja na nusu kabla ya dirisha dogo la usajili  kufunguliwa, ni muda wa wachezaji kupambania nafasi hiyo kujihakikishia nafasi ya kubaki kwani hatutakuwa na sababu ya kubaki na wakaa benchi ambao wanalipwa pesa nzuri na hawaipambanii timu.

"Wakati tunapambana na matokeo mazuri uwanjani tunatakiwa kuwa na wachezaji wapambanaji kama Kibu Denis ambaye kwasasa amekuwa muhimu kikosini akitoka tu unaona timu ikiyumba," amesema.

Try Again amesema wanataka kusajili wachezaji watakaoitumikia timu kulingana na fedha wanazopata na sio kukaa na wachezaji ambao wanalipwa fedha nyingi na hawachezi.

"Kwakuwa bado hatuna kocha hatuwezi kusajili, tunamuachia kocha nafasi hiyo kusajili wachezaji ambao wataingia kwenye mfumo wake moja kwa moja kwani tumekutana na changamoto hiyo kuna wachezaji wengi wamejikuta wanaishia benchi licha ya vipaji vyao," amesema Try Again