Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Motsepe kutua Zanzibar na ndege binafsi

MOTESEPE Pict

Muktasari:

  • Ziara hii inakuja saa chache tu, baada ya Motsepe kushuhudia mechi nyingine kubwa ya hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Mamelodi Sundowns na Pyramids ya Misri uliopigwa jijini Pretoria, Afrika Kusini. 

RAIS wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Dk. Patrice Motsepe, anatarajiwa kutua leo Jumapili  visiwani Zanzibar kwa ndege binafsi akitokea Afrika Kusini, ili ashuhudie mechi  ya fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya mwenyeji Simba na RS Berkane kutoka Morocco.

Taarifa kutoka ndani ya CAF zinaeleza kuwa, Motsepe ataongozana na wajumbe na maofisa waandamizi wa shirikisho hilo, ikiwa ni sehemu ya dhamira ya kuonyesha mshikamano na kuimarisha ushirikiano wa CAF na nchi wanachama, hasa katika mashindano ya kimataifa yanayohusisha klabu kutoka ukanda mbalimbali wa Afrika.

Ziara hii inakuja saa chache tu, baada ya Motsepe kushuhudia mechi nyingine kubwa ya hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Mamelodi Sundowns na Pyramids ya Misri uliopigwa jijini Pretoria, Afrika Kusini. 

Katika mechi hiyo, timu hizo zilitoka sare ya 1-1, huku kukiwa na ushindani mkubwa kutoka pande zote mbili, jambo lililoonyesha wazi kiwango kilichofikiwa na soka la klabu za Afrika.

Kulingana na ratiba ya awali, Motsepe anatarajiwa kuwasili Zanzibar majira ya saa 3 asubuhi na moja kwa moja kwenda katika mapumziko mafupi kabla ya jioni kutinga uwanjani kushuhudia fainali hiyo ya pili ya Kombe la Shirikisho ambayo inatarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi ndani na nje ya Tanzania. 

Baada ya mechi hiyo, Rais huyo wa CAF anatarajiwa kuondoka visiwani hapa usiku huohuo ili kuendelee na majukumu mengine.

Tayari maandalizi makubwa yamefanyika kuhakikisha ujio wake unakuwa wa heshima ya juu, huku vikosi maalum vya ulinzi vikiwa kazini kwa siku kadhaa sasa.

 Inadaiwa walinzi wa karibu wa Motsepe wamewasili Zanzibar takribani siku tatu zilizopita, wakifanya kazi ya maandalizi ya usalama katika maeneo atakayopita na atakayokaa kiongozi huyo.

Hatua hiyo inaonyesha namna CAF inavyothamini hadhi ya viongozi wake na umuhimu wa kuhakikisha usalama wao unazingatiwa katika kila nyanja.

Fainali hii ya pili kati ya Simba na RS Berkane inatarajiwa kuwa ya aina yake, si tu kwa sababu ya mvuto wa ushindani baina ya timu hizo, bali pia kutokana na uwepo wa viongozi wa juu wa CAF na wageni wengine waalikwa kutoka mataifa mbalimbali, jambo linaloifanya mechi hiyo kuwa tukio kubwa kisoka kwa Afrika Mashariki na Kati.