Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wadau watoa neno uteuzi wa Amunike

Muktasari:

Mirambo amethibitisha anaweza, lakini kitendo cha kumuongeza Amunike na kuingiza falsafa mpya ambayo kiufundi inaweza kuwachanganya wachezaji kwa kuwa siku zilizobaki ni chache kabla ya kufanyika mashindano ya Afcon.

Dar es Salaam.Muda mfupi baada ya Emmanuel Amunike kutangazwa kuongeza nguvu katika kikosi cha Serengeti Boys, wadau wa soka wametoa maoni tofauti kuhusu uteuzi huo.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidao jana alisema Amunike ataongeza nguvu Serengeti Boys licha ya timu hiyo kunolewa na Kocha Oscar Mirambo.

Miongoni mwa wadau wa soka waliotoa maoni baada ya uteuzi wa Amunike ambaye ni kocha wa Taifa Stars ni mchezaji nyota wa zamani wa Yanga, Bakari Malima.

Kauli ya wadau

Kocha wa Namungo FC Bakari Malima alisema kuongezwa kwa Amunike ni jambo jema kwa kuwa ana uzoefu wa kutosha katika soka.

“Mirambo namuelewa ni mpiganaji hakubali kushindwa, lakini atajifunza kupitia kwa Amunike ambaye hata akiondoka kuna kitu atakuwa amekiacha,”alisem Malima au Jembe Ulaya. Mwenyekiti wa zamani wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Idd Kipingu alisema uwepo wa Amunike Serengeti Boys utakuwa na manufaa.

“Unapokwenda vitani lazima utumie silaha zote ulizokuwa nazo, TFF nayo imeamua kufanya hivyo ili tupate matokeo mazuri,” alisema Kipingu.

Mchambuzi Ally Mayay alisema ana amini Amunike atachangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya Serengeti Boys kutokana na uzoefu wake kimataifa.

Mayay alisema Amunike raia wa Nigeria ana mtandao mpana katika soka ya kimataifa kwa kuwa yuko katika Kamati za Maendeleo ya Soka ya Vijana ndani ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Kimataifa (Fifa).

Hata hivyo, kauli za akina Mayay zilitofautiana na mchezaji nyota wa zamani wa Simba, Mtemi Ramadhani ambaye alisema Mirambo alipaswa kupewa jukumu zima la kuisuka Serengeti Boys kwa kuwa ameonyesha mwelekeo mzuri.

Mtemi alisema Mirambo amethibitisha anaweza, lakini kitendo cha kumuongeza Amunike na kuingiza falsafa mpya ambayo kiufundi inaweza kuwachanganya wachezaji kwa kuwa siku zilizobaki ni chache kabla ya kufanyika mashindano ya Afcon.

Tanzania itakuwa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) zilizopangwa kuanza Aprili 14 hadi 28, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa TFF Kidao alisema Amunike na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Ammy Ninje wamekwenda Arusha kuongeza nguvu katika kambi ya Serengeti Boys.