Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha JKT Tanzania awapa shavu wazawa

KOCHA Pict

Muktasari:

  • JKT Tanzania iliyomaliza nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara 2024-2025, kikosi chake kimeundwa na wachezaji wazawa pekee.

KOCHA wa JKT Tanzania, Ahmad Ally amesema kwa upande wake msimu wa 2024-25 kwa asilimia kubwa ameyaona mabadiliko kwa wachezaji wazawa kitabia na mtazamo, jambo analoamini litakwenda kuwapa manufaa.

JKT Tanzania iliyomaliza nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara 2024-2025, kikosi chake kimeundwa na wachezaji wazawa pekee.

“Wengi wao wana data kubwa, wamekuwa mfano wa kuigwa, husikii skendo ya kuwafanya waonekane watu wa ajabu na wengine wamegeuka lulu sokoni, hilo ni jambo jema ambalo litafanya timu ya taifa iwe na watu wenye viwango vikubwa,” alisema kocha huyo.

Alisema kutokana na ubora na ugumu wa ligi msimu huu, unampa picha ya kujipanga na kuhakikisha ujao 2025-2026 unakuwa wa mafanikio zaidi kwao kama wamemaliza nafasi ya sita watahitaji kupanda juu zaidi.

“Haikuwa rahisi kwa wachezaji wala makocha kuwa na muendelezo wa kufunga mechi kwa mfululizo, hilo lilitokana na udhamini ambao ulizowezesha timu kutimiza wajibu wake kirahisi, pia mabadiliko ya uendeshaji wa timu zenyewe, ndiyo maana ukiachana KenGold iliyoshuka mapema, dakika za mwisho ndipo ikajulikana Kagera Sugar nayo imeshuka na timu zinazocheza mtoano zikafahamika,” alisema.

Mechi iliyokuwa bora kwa upande wake ni dhidi ya Azam FC ya mzunguko wa kwanza ambayo ilimalizika kwa timu hizo kutoka 0-0.

“Japokuwa mchezo huo tulitoka suluhu katika uwanja wa nyumbani, lakini nilikuwa napenda mifumo ya kocha Youssouph Dabo ilifanya iwe mechi ngumu na yenye mvuto,” alisema.