Wachezaji 46 waitwa timu ya taifa, Bunda, Bilo zang'ara

Muktasari:
- Wachezaji hao wameitwa siku moja baada ya kumaliza Ligi daraja la kwanza kwa wanawake Bara
KOCHA wa timu za taifa za wanawake, Bakari Shime ameita nyota 46 kwa ajili ya mchujo wa timu za taifa huku Bunda Queens na Bilo FC zikiongoza kwa kutoa wachezaji wengi.
Wachezaji hao ni kutoka Ligi Daraja la Kwanza kwa Wanawake Bara (WFDL) ambayo imemalizika jana Aprili 23, 2023 jijini Mwanza ikishuhudiwa na kocha huyo na Rais wa Shirikisho la Soka (TFF), Wallace Karia.
Michuano hiyo iliyoshirikisha timu 14 ilianza Aprili 13 huku Bunda Queens ya Mara ikiibuka bingwa na Geita Gold mshindi wa pili ambapo timu hizo mbili zimepanda daraja kwenda Ligi Kuu.
Hata hivyo, kinara wa mabao wa Ligi hiyo, Bahati Steven aliyefunga matano hajajumuishwa kwenye kikosi hicho cha mchujo ambacho kitaanza kambi Mei Mosi, 2023 jijini Dar es Salaam.
Walioitwa ni Mariam Shaban, Melkia William, Kulwa Rocket, Sarah Lucas, Ester Maseke, Semeni Juma, Hellen Steven na Jamila Selestine kutoka Bunda Queens. Kutoka Bilo FC ni Michaela Daffa, Furaha Kifaru, Hellen Hamis, Saidath Yohana, Nusra Leonard, Amina Mussa na Jesca Bernad.
Kutoka Geita Gold Queens ni Naomi Samwel, Restuta Innocent, Sabina Alex, Sarafina Thadey, Saada Mabere, Allie Sebastian, Mariam Salum, Sabina Alex na Marry Elia. Pia wamo, Winfrida John, Glory Ibrahim na Edina Madamba wa Oyesterbay Queens.
Wengine ni, Mwanaidi Maulidi, Yusta Zonobia, Farida Abdallah, Lidya Maximilian wa TSC Queens, Kurwa Nkwabi na Fatuma Abdallah (Ukerewe), Marry Joseph, Rukia Hussein na Adrophina Michael (Ruangwa).
Pia wamo Happiness Daffa (Masala), Diva Godrey (Mapinduzi), Angel Wilbert na Petronila Simon (Lengo) na Saada Ayoub (JMK Park).
Timu nyingine zilizotoa wachezaji kwenye kikosi hicho ambazo hazikushiriki daraja la kwanza ni Mabibo Queens (Eva Elikana na Maria Jusel), Mbagala Queens (Zuhura Hamsin na Hidah Suleiman), Sayari Queens (Mage Ageth) na Kinondoni Queens (Sundi Ramadhan)