Waalgeria, Mamelodi kukipiga bila mashabiki kwa Mkapa

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

Waarabu wametaka mchezo wao kuchezwa bila mashabiki.

KLABU YA CR Belouizdad ya Algeria ni kama imewakomalia wapinzani wao, Mamelod Sundowns baada ya kutaka mchezo wao kuchezwa bila mashabiki.

Belouizdad na Mamelod Sundowns watacheza mchezo huo Jumapili keshokutwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10: jioni.

Belouizdad ndio wenyeji wa mchezo huo baada ya kuomba kuutumia uwanja wa Benjamin Mkapa kama uwanja wao wa nyumbani hivyo wana haki ya kuamua kama ilivyokuwa kwa CD de Agosto walivyocheza na Namungo kwenye mchezo wao bila mashabiki.

Kupitia katika taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Ndimbo  imesema kuwa;  "Watazamaji hawatoruhusiwa katika mchezo huu kwa kuwa ni utaratibu uliopangwa na wenyeji toka awali".

Hata hivyo awali baadhi ya viongozi wa Mamelod Sundowns waliomba sapoti ya mashabiki wa Simba kupitia kwa Mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez.

Timu mbalimbali zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa na Shirikisho Afrika zimekuwa zikitumia viwanja tofauti na vyao kutokana na nchi nyingi kukumbwa na janga la ugonjwa COVID 19.