Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Viongozi Alliance chanzo kupigwa mkono na Simba

Muktasari:

Alliance FC ikicheza bila ya kocha wake Kocha Mkuu Mbwana Makata pamoja na msaidizi Renatus Shija  ilikubali kipigo cha mabao 5-1 kutoka kwa Simba na kuzidi kukaa katika mazingira mabaya ya kushuka daraja.

 

MWANZA. Achana na kichapo cha mabao 5-1 ilichopa Alliance FC kutoka kwa Simba, imebainika kuwa nyuma yake hali si shwali kati ya Uongozi na Benchi la Ufundi na ndio sababu ya matokeo hayo.

Alliance ikiwa ni msimu wake wa kwanza kushiriki Ligi Kuu imekuwa na mwenendo usioridhisha kwani kati ya mechi 11 ilizocheza imeshinda mchezo mmoja, sare tatu na kupoteza saba na kukaa mkiani.

Jana ikicheza kwenye Uwanja wa Taifa bila Makocha wake watatu, Mbwana Makata, Kessy Mzirai na Renatus Shija ilikumbana na kipondo hicho kutoka kwa Simba ikiwa ni siku chache tangu ilipotandikwa mabao 3-0 na Yanga.

Kocha Mkuu Mbwana Makata alisema kabla ya mchezo dhidi ya Simba, Benchi la Ufundi waliandaa wachezaji ambao watatumika lakini baadaye uongozi ukaja na kikosi chao.

Alisema kuwa baada ya kuona hivyo yeye pamoja na wenzake waliona isiwe taabu wakaamua kuwaachia timu viongozi ili wapambane na kilichotokea wao hawahusiki.

“Ni mambo ya kawaida tu, lakini sisi tuliona isiwe tatizo kwetu kwa sababu kabla ya mchezo tuliandaa kikosi kulingana na mechi yenyewe, lakini tulishangazwa kuona wao wanakuja na kikosi chao kwahiyo tukaona tuwaachie wapambane,”alisema Makata.

Kocha huyo aliongeza kuwa suala la kubaki klabuni humo au kuachana nayo itajulikana baadaye baada ya kumaliza jambo hilo lilijitokeza jana Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Yusuph Budodi alisema kuwa kwa sasa (jana) hawawezi kulizungumzia jambo hilo kwani ni mlolongo mkubwa na kusema kuwa watalifafanua kesho Ijumaa ili umma ujue.

“Ndio tupo safari tunakuja Mwanza, kwahiyo ninaomba tukifika tutalizungumza kwa mapana kwa sababu ni historia ndefu naomba kesho tutazungumza na waandishi wa habari ili umma ujue,” alisema Budodi ambaye pia ni Meneja Msaidizi wa Klabu hiyo.