Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Stand United, Fountain Gate kitawaka Shinyanga

STAND Pict

Muktasari:

  • Chama la Wana linapambana kutaka kurejea Ligi Kuu kuungana na Mtibwa Sugar na Mbeya City zilizotangulia mapema, wakati Fountain inapambana kuepuka kushuka daraja kuzifuata KenGold na Kagera Sugar zilizoshindwa kushikilia bomba.

VITA ya kuisaka tiketi ya kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao inaendelea leo kwa mechi ya play-off kati ya wenyeji Stand United ya Ligi ya Championship na Fountain Gate ya Ligi Kuu Bara, itakayopigwa kwenye Uwanja wa Kambarage, mjini Shinyanga.

Chama la Wana linapambana kutaka kurejea Ligi Kuu kuungana na Mtibwa Sugar na Mbeya City zilizotangulia mapema, wakati Fountain inapambana kuepuka kushuka daraja kuzifuata KenGold na Kagera Sugar zilizoshindwa kushikilia bomba.

Stand iliyomaliza katika nafasi ya tatu katika Ligi ya Championship imefikia hatua hiyo baada ya kuiondoa Geita Gold iliyomaliza ya nne ikiifunga mabao 4-2 katika mechi za mtoano.

Kwa Fountain iliyomaliza nafasi ya 14 katika Ligi Kuu imeangukia hapo baada ya kutandikwa pia mabao 4-2 na Tanzania Prisons katika mechi za mtoano kwa timu za Ligi Kuu na sasa inajiuliza kama inataka kusalia kwa msimu ujao au iipishe Stand.

Stand inayopambana kurejea Ligi Kuu baada ya kushuka msimu wa 2018-19, itaendelea kuwategemea nyota wa timu hiyo, Omary Issa ‘Berbatov’ aliyemaliza na mabao tisa katika Ligi ya Championship na Emmanuel Manyanda aliyefunga manane.

Wengine ni Seleman Richard na Msenda Msenda waliomaliza na mabao saba kila mmoja na kuifanya timu hiyo kuongeza ushindani, nyuma ya Mbeya City iliyomaliza ya pili na Mabingwa wa Championship Mtibwa Sugar zilizopanda Ligi Kuu.

Kwa upande wa Fountain, itaendelea kuwategemea nyota wa kikosi hicho, Edgar William aliyemaliza msimu akiwa na mabao sita pamoja na kiungo mshambuliaji kinara wa mabao wa kikosi hicho Mrundi Elie Mokono aliyefunga saba.

Akizungumza na Mwanaspoti, kocha wa Stand, Juma Masoud (pichani) alisema anatarajia mechi ngumu na ya ushindani kutokana na uhitaji wa kila timu, ingawa anachokitaka ni kuhakikisha wachezaji wanajituma ipasavyo na kutumia pia faida ya nyumbani.

“Tumekuwa na muda mrefu wa maandalizi japo hatujapata mechi za kiushindani tofauti na wenzetu walioendelea kucheza, tunahitaji kuonyesha nidhamu ya kiuchezaji kwa maana ya kujilinda vizuri na kushambulia pia,” alisema.

Kocha wa Fountain, Mohamed Ismail ‘Laizer’, alisema makosa mbalimbali ikiwamo ya kujilinda yaliyotokea mechi ya mwisho dhidi ya Prisons ameyafanyia kazi kwa kiwango kikubwa, japo atahakikisha anapambana ili kulinda heshima yake.

“Siko tayari kuona timu hii ikishuka nikiwa mkuu wa benchi la ufundi, nitapambana hadi tone la mwisho, katika mechi hii tutamkosa kipa Machupa Kilusumo aliyepata kadi nyekundu dhidi ya Tanzania Prisons ila wote wako fiti,” alisema Laizer.