Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usyk ampa neema Anthony Joshua

Usyk ampa neema Anthony Joshua

Muktasari:

  • Hilo ni pambano la tatu Joshua kupigwa kati ya mapambano 27 aliyocheza, ameshinda 24 (22 kwa KO), amepigwa na Usyk mara mbili mfululizo zote kwa pointi na Andy Ruiz kwa TKO, hajawahi kutoka sare.

ACHANA na kipigo cha pointi za majaji 2-1 alichokutana nacho Muingereza, Anthony Joshua mbele ya Oleksandr Usyk usiku wa kuamkia jana Jumapili, matokeo hayo yamekuwa na neema kwa Joshua.

Iko hivi, kabla ya pambano hilo lililopigwa huko Jeddah, Falme za Kiarabu, Joshua au AJ kama amnavyopenda kujiita alikuwa ni bondia namba tatu kwa ubora duniani kwenye uzani wa juu.

Matokeo ya pointi na Usyk bondia namba moja duniani kwenye uzani wa juu yamemuongezea pointi AJ na kupanda hadi nafasi ya pili akimshusha Mmarekani, Deontay Wilder ambaye sasa yuko kwenye tatu nyuma ya mbabe, Usyk ambaye amezidi kujiimarisha kileleni baada ya pambano la juzi usiku.

Jaji Glenn Feldman pekee alimpa ushindi wa pointi 115-113 Joshua huku Viktor Fesechko aliyetoa pointi 116-112 na Steve Gray aliyetoa pointi 115-113 wakimpa ushindi Usyk aliyetetea mataji ya IBF, IBO, WBA na WBO, matokeo ambae yameendelea kumfanya kuwa namba moja duniani kwenye uzani wa juu, lakini pia yakimneemesha Joshua ambaye ameongeza pointi kadhaa kwa mujibu wa mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia (Boxrec).

Kama angepigwa, Usyk (35) raia wa Ukraine anayeishi Marekani angeporomoka na huenda angempisha Joshua kwenye namba moja ya dunia, jambo ambalo hakuruhusu litokee baada ya kutetea mataji yote manne lakini pia yakimpandisha pia Joshua (32) hadi nafasi ya pili na Deontay Wilder (36) akiporomoka kwa nafasi moja na sasa ni bondia namba tatu duniani kwenye ubora katika uzani wa juu.

Hata hivyo, Muingeraza mwingine, Tyson Furry ambaye Usyk ana ndoto za kuzichapa naye hayupo kwenye renki ya mabondia bora wa uzani wa juu ingawa hivi karibuni alitwaa ubingwa na kutangaza kustaafu, japo kuna uwezekano akabatilisha uamuzi wake wa kustaafu na kurejea tena ulingoni.