Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uchaguzi Simba waingiza fedha

Muktasari:

  • Takwimu ambazo Mwanaspoti imezipata na kuthibitishwa na Katibu Msaidizi wa Kamati ya Uchaguzi huo, Amani Kamguna, zinaonyesha kuwa wagombea 41 wamejitokeza kuchukua fomu hizo na kulipa ada ambazo jumla yake ni Sh9.7 milioni

MAMBO ya fedha hayo. Zoezi la kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongizo wa klabu ya Simba lilikamilika juzi Jumatano huku likikusanya Sh9.7 milioni zikiwa ni ada za uchukuaji fomu kutoka kwa wagombea.

Takwimu ambazo Mwanaspoti imezipata na kuthibitishwa na Katibu Msaidizi wa Kamati ya Uchaguzi huo, Amani Kamguna, zinaonyesha kuwa wagombea 41 wamejitokeza kuchukua fomu hizo na kulipa ada ambazo jumla yake ni Sh9.7 milioni.

“Wagombea waliojitokeza ni wengi ingawa tulitarajia kuwa wangezidi zaidi ya hapo, huenda ni kutokana na kiwango kilichopangwa cha kulipia fomu kwani kinaonekana kikubwa, ndiyo maana hawajajitokeza wengi zaidi ya hapa,” alisema Kamguna.

Wagombea watatu wa nafasi ya Rais walijitokeza kuchukua fomu ambao ni Michael Wambura, Evance Aveva na Andrew Tupa. Kwa nafasi hiyo, kila mmoja wao amelipia ada ya Sh500,000 hivyo kufanya jumla ya Sh1.5 milioni.

Nafasi ya Makamu Rais wamejitokeza wagombea sita ambao ni Swed Nkwabi, Joseph Itang’are ‘Mzee Kinesi’, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, Bundala Kabulwa, Wilbar Mayage na Jamhuri Kihwelo  ‘Julio’ ambao kila mmoja amelipa Sh300,000, hivyo wote kutoa kiasi cha Sh1.8 milioni.

Katika nafasi ya ujumbe, kuna wagombea 32 ambao kila mmoja amelipa kiasi cha Sh200,000 na kukusanya jumla ya Sh6.4 milioni. Wagombea ujumbe hao ni George Wakuganda, Said Tulli, Damian Manembe, Said Pamba, Abdulhamid Mshangama, Alfred Elia, Ally Suru, Ramson Rutiginga, Seleman Dewji, Idd Kajuna, Khamis Mkoma na Rodney Chiduo.

Wengine ni Collin Frisch, Juma Pinto, Chano Hassan, Emmanuel Kazimoto, Salim Jaza, Amina Poyo, Yassin Mwete, Hussein Simba, Ally Chaurembo, Ibrahim Masoud, Ahmed Mlanzi, Iddy Mkambala, Kessy Kikoti, Maulid Abdallah, Juma Mussa, Asha Muhaji, Omary Said, Said Kubenea, Asha Kigundula na Jasmin Badar.

Kwa mujibu wa Kamguna, kiasi hicho cha fedha kimezidi kile kilichokusanywa katika uchaguzi uliopita mwaka 2010 ambao uliingiza Sh4.6 milioni tu. Hata idadi ya wagombea safari hii imezidi kwani mara ya mwisho kulikuwa na wagombea 32. Uchaguzi wa mwaka huu unatarajiwa kufanyika Juni 29.

Katika uchaguzi uliopita, wanachama sita walijitokeza kuwania uenyekiti (sasa urais) wa klabu, wawili nafasi ya makamu mwenyekiti (makamu wa rais kwa sasa) na wanachama 24 wakijitokeza kugombea nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji.