TPLB yaufungia Uwanja wa Liti, sababu zatajwa

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeufungia Uwanja wa Liti uliopo mjini Singida unaotumiwa na klabu ya Singida Fountain Gate kama uwanja wa nyumbani kutokana na kukosa vigezo vya kikanuni na Sheria za mpira wa miguu
Taarifa inasema “Eneo la kuchezea (pitch) la Uwanja huo halifai kuchezewa mpira kutokana na eneo hilo kutokuwa na nyasi kijani sehemu kubwa ya uwanja kamailivyoanishwa kwenye masharti ya kanuni ya leseni za klabu."
“Kufuatia uamuzi huo timu ya Singida amabyo inatumia Uwanja huo kwa michezo yake ya nyumbani italazimika kutumia uwanja mwingine kama kanuni inavyoelekeza mpaka uwanja wao utakapofunguliwa, baada yakufanyiwa marekebisho na kukaguliwa na kamati ya leseni za klabu TFF.
TFF inaendelea kuzikumbusha klabu za Ligi Kuu Bara, Ligi ya Championship na First League kuendelea kuboresha na kutunza miundombinu ya viwanja vyao vya nyumbani kwa kushirikiana na wamiliki wa viwanja hivyo (kwa klabu ambazo hazimliki viwanja) ili michezo ya Ligi ichezwe kwenye viwanja bora vinavyosaidia kuongeza ushindani na thamani ya Ligi
Mara ya mwisho Uwanja huo ulitumika jana Disemba1, katika mchezo wa raundi ya 13 kati ya wenyeji Singida dhidi ya JKT Tanzania uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.