Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mokwena, Yanga ngoma nzito

MOKWENA Pict

Muktasari:

  • Hesabu za Yanga zilikuwa kwa makocha watatu bora, ilianza na Marcel Koller aliyekuwa Al Ahly ya Misri lakini inaelezwa jamaa alichomoa akitaka kupumzika huku akiwa na ofa kubwa kutoka Asia.

YANGA inaendelea kupasua kichwa juu ya kocha gani imchukue kwa ajili ya kulijenga upya benchi la ufundi la msimu ujao, na sasa ni kwamba kuna uwezekano mkubwa ikapoteza chaguo jingine la tatu kwenye mawindo hayo.

Hesabu za Yanga zilikuwa kwa makocha watatu bora, ilianza na Marcel Koller aliyekuwa Al Ahly ya Misri lakini inaelezwa jamaa alichomoa akitaka kupumzika huku akiwa na ofa kubwa kutoka Asia.

Nje ya Koller Yanga ikamrukia Jose Riveiro aliyekuwa kocha wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini aliyechukuliwa fasta na Al Ahly ya Misri aliyeenda kuziba nafasi ya Koller kwa wababe hao.

Kumbuka msimu huu Ahly ilikuwa kundi moja na Orlando katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Mreno huyo alivuna pointi nne mbele ya timu hiyo kutoka Misri, ikiwamo sare nyumbani kisha kushinda 2-1 ugenini katika hatua ya makundi.

Baada ya hapo Yanga ikatua kwa Rhulani Mokwena aliyewahi kuzinoa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Wydad Casablanca ya Morocco waliotemana hivi karibuni, ambaye kwa mujibu wa mabosi wa Yanga mazungumzo yalikuwa yanakwenda vizuri lakini wiki iliyopita mambo yakabadilika kutokana na masharti aliyoyatoa kocha huyo raia wa Afrika Kusini.

Hata hivyo, Yanga imezipata taarifa kuwa Mokwena anafanya mazungumzo pia na Zamalek ya Misri huku akiwapa masharti kuwa mshambuliaji wa Jangwani, Clement Mzize anataka uwe usajili wake wa kwanza mara atakapotua huko kwa mabingwa hao wa Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita.

Zamalek inamtaka Mzize ambaye amewahi pia kutakiwa na Mokwena aliyemsifu kuwa ni mshambuliaji mzuri wakati akizifundisha Mamelodi na Wydad.

“Kuna masharti tulikuwa tunapambana nayo, lakini hapa kati hasa wiki iliyopita amekuwa na ugumu kukubaliana na baadhi ya tunayotaka nasi ila tumepata taarifa kwamba anatakiwa pia na Zamalek na wapo hatua kubwa zaidi. Hii ni moja ya ilivyochangia hali hii,” alisema bosi huyo wa juu ndani ya Yanga.

Endapo Yanga itamkosa Mokwena itabaki na chaguo la nne ambalo ni kocha wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Jullien Chevalier ambaye tayari alishaanza mazungumzo na vinara hao wa Ligi.

Kocha huyo Mfaransa ndiye aliyewapika kina Stephane Aziz Ki, Yao Kouassi na Pacome Zouzoua waliosajiliwa na Yanga kabla Aziz Ki hivi karibuni kusajiliwa na Wydad, inalezwa ameomba kuondoka ASEC baada ya kuinoa kwa misimu minne kwa mafanikio makubwa.