Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kigwangalla ammwagia maua MO Dewji, Simba

KIGANGWALA Pict

Muktasari:

  • Simba imefika fainali ya Kombe la Shirikisgho Afrika msimu huu na inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 72.

Mwanachama mwandamizi wa Simba na Mbunge wa Nzega Vijijini, Dk Hamis Kigwangalla amefurahishwa na maendeleo ya timu hiyo huku akisema kwa sasa anakoshwa na utendaji kazi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Bilionea Mohammed Dewji.

Kigwangalla ametoa kauli hiyo akipinga taarifa feki iliyotolewa na ukurasa wa X uliojitambulisha kwa jina lake ukimlaumu Dewji kwa kudai ndio chanzo cha Simba kutotwaa mataji msimu huu.

"Huu siyo mwandiko wangu. Kwanza mimi binafsi nimeridhishwa sana na uchezaji wa timu yetu msimu huu, sina malalamiko wala siwadai vijana wetu wa Nguvu Moja!. Aidha, mimi siwezi kutumia lugha zenye kuashiria ubaguzi wa rangi kwa mtu yeyote yule. 

"Kufungwa ni matokeo tu. Lakini kiukweli kocha na wachezaji wametuheshimisha sana, kuwalaumu ni kuwa na moyo usio na shukran. Ama kuhusu hiyo post, sijaiandika mimi. Sipo Twitter kwa zaidi ya miezi mitano sasa!.

"Halafu, mwekezaji wetu siku hizi ametulia, hana kelele nyingi. Siwezi kuwa mchokozi kumchokonoa, kama yeye mwenyewe ameamua kutulia na kufanya kazi kistaarabu na kwa weledi. Wanasimba kuweni makini kuelekea derby kuna mengi tutasikia, kuna mengi tutaona. Tusiyumbe wala tusiyumbishwe. Umoja wetu ndiyo nguvu yetu," amesema Kigwangalla.

Kigwangalla anakumbukwa kwa hoja zake za kukosoa uwekezaji wa Dewji ambapo mara kwa alikuwa akidai kuwa Bilionea huyo anaitumia Simba kujinufaisha.

Tamko hilo la Kigwangalla limeonekana kuwakosha mashabiki wengi wa Simba ambao wametumia ukurasa wa Instagram wa mbunge huyo kumpongeza.