Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Township Rollers yapiga mtu nne yatwaa ubingwa

Muktasari:

Kocha wa timu hiyo ameweka wazi msimu huu lengo lake kubwa ni kufuzu kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa

Gaborone, Botswana. Township Rollers imeitumia Yanga salamu baada ya kutwaa ubingwa wa Mascom Top 8 kwa kuichapa Orapa United 4-2, katika fainali iliyofanyika kwenye Uwanja wa Francistown Sports Complex.

Township Rollers inategemea kuingia Tanzania kesho jioni au Jumatatu asubuhi tayari kwa mchezo wake wa kwanza wa hatua ya mtoano ya kusaka kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Yanga.

Wakati Yanga ikiomba kupumzika kucheza mechi ya ya Ligi Kuu wiki hii ili kujiandaa hali ilikuwa ni tofauti kwa wapinzani wake Rollers ambao leo jioni ilicheza mechi yake ya fainali na kuchukua ubingwa wake wa kwanza nchini Botswana.

Townships ilitawala mchezo wake wa fainali kwa kupata mabao manne ya haraka kupitia kwa Lemponye Tshireletso, Edwin Moalosi, Bogosi Nfila na Kaone Vanderwesthuizen kabla ya kuruhusu mabao mawili ya wapinzani wake Orapa yaliyofunga katika dakika 20 za mwisho kupitia Omaatla Kebatho na Gift Moyo.

Kocha wa Rollers, Nikola Kavazovic alifanya mabadiliko ya kikosi chake chote kutoka kile kilichofungwa na BDF XI Jumatatu iliyopita katika Ligi Kuu.

Kavazovic alimwazisha golini Keeagile ‘Skheza’ Kgosipula, pia akitumia mfumo wa 4-4-2 akiwa na wachezaji wake Tshepo ‘Talk Talk’ Motlhabankwe, Galabgwe ‘Galaxy’ Moyana Mosha ‘Fanta’ Gaolaolwe, Simisani ‘Inspector’ Mathumo, Ofentse ‘Size 10′ Nato, nahodha Maano ‘Abutreka’ Ditshupo, Motsholetsi ‘Viva’ Sikele, Segolame ‘Smatsatsa’ Boy, Edwin ‘Moluba’ Moalosi na Lemponye ‘FC’ Tshireletso.