Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba kuvuta mtu Mauritania

MAURITANIA Pict

MABOSI wa Simba wameanza kuboresha kikosi kwa ajili ya msimu ujao ili kuongeza ushindani, huku suala la makipa likiwa kitendawili kutokana na kuripotiwa kutaka kuachana na Moussa Camara, jambo ambalo limewapeleka hadi Mauritania kupambana kunasa saini moja matata.


Camara aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea Horoya AC ya kwao Guinea, inaelezwa huenda akaachana na Simba kutokana na makosa anayofanya, licha ya kuongoza kwa ‘clean sheets’ - nyingi zaidi za Ligi Kuu akiwa nazo 19.


Wakati hayo yakiendelea, mabosi wameanza kutafuta mbadala wa kipa huyo, huku taarifa ambazo Mwanaspoti limezipata miongoni mwao ni Issa Fofana anayeichezea Al-Hilal Omdurman ya Sudan.

Chanzo kinasema Fofana ambaye ni raia wa Ivory Coast ni miongoni mwa makipa bora kwa sasa na tayari ameshaonyesha kiwango kizuri, jambo linalowafanya mabosi wa Simba kumpigia hesabu za msimu ujao ikiwa Camara ataondoka kikosini.

“Ni kipa mdogo ambaye tayari ameonyesha kiwango kizuri na tunategemea kuanza kufuatilia upatikanaji wake, tukiamini ni chezaji atakayeleta mapinduzi makubwa ya kiuchezaji kwa sababu anajua kucheza soka la kisasa,” kilisema chanzo hicho.

Fofana aliyejiunga na Al Hilal Agosti 13, 2022, akitokea San Pedro ya Ivory Coast mkataba wake na kikosi hicho unafikia tamati Juni 30, 2025, jambo linalowafanya mabosi wa Simba kumpigia hesabu mapema.

Kipa huyo ameiwezesha Al Hilal chini ya Kocha Florent Ibe-nge, ili- yoshiriki Ligi Kuu  Mauritania ‘Ligue 1’ msimu huu kutwaa ubingwa  baada ya kucheza mechi 30 ikishinda 20, sare saba na kupoteza mitatu, ikiongoza na pointi 67.
Al Hilal na Al Merrikh iliyomaliza nafasi ya sita na pointi 44 ziliomba kushiriki Ligue 1 kutokana na usalama mdogo kwao Sudan.

Hata hivyo, wakati mabosi wa Simba wakimpigia hesabu kipa huyo wanakumbana na changamoto nyingine ambapo inaelezwa huenda wakamrudisha kundini Ayoub Lakred baada ya kupona majeraha jambo lililosababisha kuondolewa kwenye mfumo.

Lakred aliyejiunga na Simba Agosti 11, 2023 akitokea FAR Rabat ya kwao Morocco, mkataba wake pia unaisha Juni 30, 2025 jambo linaloongeza ugumu wa kuongezewa mwingine kutokana na kutopata muda mrefu wa kucheza kikosini.

Jambo linalosumbua vichwa vya mabosi wa Simba kwa sasa ni kutafuta kipa mwingine kama ataondoka Camara, ingawa Lakred pia ni ngumu kusalia kutokana na taarifa kuwa Morocco anawindwa na timu za kwao.

Ukiachana na hilo, jambo lingine linalowauma mabosi wa Simba ni ikiwa sheria ya usajili wa kipa mmoja wa kigeni msimu ujao itapita kama ambavyo Februari 12, 2025, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia alivyonukuliwa.

“Kuanzia msimu ujao tunakuja na kanuni ya kipa mmoja tu wa kigeni kwenye kila timu. Haiwezekani kwenye klabu moja kuwe na makipa wawili wa kigeni. Haiwezekani hii,” alinukuliwa Karia akimaanisha makipa wazawa wapate pia nafasi.

“Nilikuwa namtania rais mwenzangu wa shirikisho aliniambia mbona kwenye ligi yako kuna wachezaji wa kigeni wengi sana. Nikamjibu siwadekezi watu wavivu ukiangalia pale Yanga kuna mabeki wengi wakizawa ndio wanacheza hata Simba pia hivyo hivyo.” 

Ikiwa sheria hiyo ya kipa mmoja wa kigeni msimu ujao itapitishwa na kuanza kutumika, itakuwa pigo kwa timu nyingi zaidi za Ligi Kuu Bara zenye uwezo wa kuwasajili, ingawa itakuwa chachu ya wazawa kupambana na kuongeza ushindani wanapocheza vikosini.