Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aziz KI amtaja Pacome Marekani

AZIZ KI Pict

WAKATI timu anayoichezea sasa ya Wydad Casablanca ya Morocco ikiaga fainali za Kombe la Dunia la Klabu, kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki amevunja ukimya akazungumza na Mwanaspoti kutokea Marekani.


Unaambiwa kwamba mchezaji huyo ambaye aliondoka Yanga akiwa na faida nyingi ikiwamo kumuoa binti mrembo wa Kitanzania, mwanamitindo Hamisa Mobetto, kaiambia Mwanaspoti kwamba kuna jambo ambalo halijamshangaza Bara, lakini akimtaja Pacome hukohuko.


Aziz KI ameizungumzia Dabi ya Kariakoo iliyopigwa Jumatano akisema haikumshangaza Simba kufungwa, huku akimtaja Pacome Zouzoua.

Yanga ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba katika mechi ya Dabi ya Kariakoo iliyoahirisha mara mbili - Machi 8 na Juni 15 - na kubeba ubingwa kwa mabao ya Pacome aliyefunga kwa penalti na Clement Mzize aliyetumia asisti ya kiungo mshambuliaji huyo aliyeibuka nyota wa mechi.

Kumbe wakati Yanga ikiwa uwanjani, Aziz KI alikuwa akiufuatilia mchezo huo na kukiri mziki wa Pacome upo juu mno, pia hakushangaa kuona Simba ikipasuka kwani ilizidiwa mbali na wapinzani wao kwa viwango vya mchezaji mmoja mmoja na hata kitimu kwa ujumla.

Akizungumza na Mwanaspoti, Aziz KI amesema hakuwa na shaka kabisa na Yanga hasa kwenye suala la kuifunga Simba.

Amesema tangu mchezo ulipoahirishwa alijua tu kuwa nafasi bado ipo kutokana na kikosi kipana ilicho nacho timu hiyo.

“Yanga ninayoifahamu ndio nimeiona katika mechi ya juzi (Jumatano) bila kipingamizi ina kikosi bora sana ambacho kimeonyesha ukubwa wake. Simba ilijichelewesha tu yenyewe kwani hata ingecheza na sisi wakati wowote wanaoutaka bado tungeishinda,” amesema Aziz KI.

Kuhusu Pacome, amesema amefurahishwa na mastaa wa Yanga lakini zaidi alikuwa Pacome kwa jinsi alivyoonyesha ubora ule anaoufahamu tangu wakiwa Ivory Coastal.

“Pacome ndiye mchezaji hatari zaidi ambaye nimemuacha Yanga. Kwa sasa atasumbua zaidi na kwa juzi ndio nimeanza kuona ubora wake halisi ambao ninaujua,” amesema Aziz aliyechangia mabao tisa na asisti saba kabla ya kuuzwa Wydad hivi karibuni alikoshiriki fainali za Kombe la Dunia la Klabu zinazoendelea Marekani na timu hiyo kutolewa bila kuonja ushindi hata mmoja katika mechi tatu.

Kwa msimu huu Pacome amehusika na mabao 22 akifunga 12 na kuasisti 10 tofauti na uliopita alipofunga mabao saba na asisti tatu ikiwa na maana alihusika na mabao 10 katika Ligi Kuu kabla ya kuumia na kushindwa kumalizia msimu.

Kupitia Mwanaspoti kocha wa mastaa hao wa zamani kutoka Asec Mimosas, Julien Chevalier amesema kuwa kuondoka kwa Aziz KI ndani ya Yanga kutampa nafasi Pacome kucheza nafasi anayoiwezea kwa upana zaidi na moto wake utaonekana.

Aziz Ki ameondoka Yanga akiwa mfungaji bora wa msimu uliopita aliofunga mabao 21 na asisti nane na kuiwezesha timu hiyo kutetea taji kwa msimu wa tatu mfululizo mbali na kuipa Kombe la Shirikisho (FA) na Ngao ya Jamii, lakini msimu huu wababe hao wa mitaa ya Jangwani na Twiga wamefanikiwa kutetea taji kwa mara ya nne, na Jumapili wanacheza fainali ya Kombe la Shirikisho ambayo Aziz amefunga mabao manne kabla ya kuondoka kikosini.