Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TFF:Tuko hatua za mwisho kuongeza nguvu benchi la Ufundi Serengeti

Muktasari:

Timu ya Serengeti imekuwa ikinolewa na kocha Milambo kwa muda mrefu, hadi sasa inapojiandaa kushiriki Afcon ya vijana itakayofanyika nchini ndipo TFF imeamua kumuongezea nguvu kocha Milambo.

Arusha.Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeweka wazi mipango ya kuongeza nguvu kwenye benchi la ufundi la timu ya Soka ya vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) itakayoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana (Afcon U17).

Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau alisema wako kwenye hatua za mwisho kumleta kocha ambaye atasaidiana na kocha mkuu, Oscar Milambo.

"Mazungumzo yetu na kocha huyo yako katika hatua za mwisho ili kuanza kazi," alisema Kidau na kufafanua. "Kocha huyo atakuja kama mshauri wa benchi la ufundi ambaye atasaidia na Milambo.

Hata hivyo Kidau alikataa kumtaja jina kocha huyo wala anakotokea kama ni mzawa au ni wa kutoka Nje ya nchi akisisitiza hadi atakapotambulishwa ndipo itajulikana.

Timu ya Serengeti imekuwa ikinolewa na kocha Milambo kwa muda mrefu, hadi sasa inapojiandaa kushiriki Afcon ya vijana itakayofanyika nchini ndipo TFF imeamua kumuongezea nguvu kocha Milambo.