Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Taoussi siku zinahesabika Azam

TAUSI Pict

Muktasari:

  • Katika mechi 28 ilizocheza Azam hadi sasa imeshinda 17, sare sita, imepoteza tano, ikifunga mabao 48 na kufungwa 17 ikishika nafasi ya tatu kwa kukusanya jumla ya pointi 57 na ikiwa imeshakata tiketi ya CAF kwa michuano ya Kombe la Shirikisho sambamba na Singida Black Stars iliyopo ya nne.

AZAM FC inaendelea kujifua kwa ajili ya mechi mbili za kumalizia msimu ikiwamo dhidi ya Tabora United na ile ya Fountain Gate, lakini mabosi wa klabu hiyo wameanza mapema mipango kikosi hicho kuanzia kwa wachezaji hadi benchi la ufundi na siku za kocha Rachid Taoussi kwa sasa zinahesabika.

Taarifa ambazo Mwanaspoti imepenyezewa kutoka kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu msimu wa 2013-2014 ni kuna wachezaji kadhaa wapya wameshasainishwa mikataba kimyakimya na tayari mabosi wameamua kutoendelea na kocha Taoussi mara baada ya mkataba wake kumalizika.

Kocha huyo alijiunga na Azam msimu huu kwa mkataba wa mwaka mmoja, huku cv yake ikionyesha amewahi kuzifundisha klabu kubwa Afrika kama Wydad AC na Raja Casablanca za Morocco na timu ya taifa ya Morocco kwa vipindi viwili ikiwemo mwaka 2014 alipofungwa mabao 3-1 na Taifa Stars.

Chanzo cha kuaminika kutoka Azam, kimesema uongozi umeanza mchakato wa kusaka kocha mpya atakayeweza kutimiza malengo ya klabu hiyo na hasa kufanya vizuri katika michuano ya Kombe la Shirikisho msimu ujao wakitaka kuondokana na kuwa wasindikizaji kila walishiriki CAF.

Inaelezwa, Azam inapiga hesabu za kutaka angalau kutinga makundi ya michuano hiyo kutokana na ukweli tangu imeanza kushiriki michuano ya CAF mwaka 2015 haijawahi kufika hatua hiyo, licha ya kuwa na wachezaji na makocha wakubwa kila msimu na msimu huu ilitolewa raundi ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa na APR ya Rwanda kwa jumla ya mabao 2-1.

“Kocha Taoussi akimaliza kusimamia mechi mbili zilizosalia dhidi ya Tabora United na Fountain Gate basi tutakuwa tumemalizana naye tutampa mkono wa kwaheri nasi tuendelee na maisha mengine,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Tunahitaji marekebisho makubwa kikosini kujiandaa na michuano ya CAF, tunaamini tukijipanga tutafanya vizuri kwa msimu ujao, ukiacha kocha tusajili wachezaji wapya wa kuongeza nguvu kikosini.”

Katika mabadiliko ambayo Azam imeanza kuyafanya ni kumsajili kipa Aishi Manula aliyekuwa Simba ili kwenda kuchukua nafasi ya Msudan Mohamed Mustafa, pia ikimnasa kiungo aliyekuwa akicheza Misri, Muhsin Malima, huku ikisaka mbadala wa mshambuliaji Gibril Sillah mwenye mabao tisa anayedaiwa kumalizana na Yanga.

Katika mechi 28 ilizocheza Azam hadi sasa imeshinda 17, sare sita, imepoteza tano, ikifunga mabao 48 na kufungwa 17 ikishika nafasi ya tatu kwa kukusanya jumla ya pointi 57 na ikiwa imeshakata tiketi ya CAF kwa michuano ya Kombe la Shirikisho sambamba na Singida Black Stars iliyopo ya nne.