Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania vitani mbio za magari ubingwa Afrika

Muktasari:

  • Watanzania  wanachuana na madereva wengine 51 kutoka nchi za Kenya, Rwanda, Ethiopia na wenyeji Uganda katika mashindano ambayo yanachezwa kwa mara ya kwanza magharibi ya Uganda katika maeneo ambayo Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametokea.

MADEREVA wa Tanzania, Yassin Nasser na Prince Charles Nyerere wanaingia vitani leo mjini Mbarara ambako raundi ya pili ya mashindano ya mbio za magari ubingwa wa Afrika yanaanza kwa mbio za mchujo.

Watanzania  wanachuana na madereva wengine 51 kutoka nchi za Kenya, Rwanda, Ethiopia na wenyeji Uganda katika mashindano ambayo yanachezwa kwa mara ya kwanza magharibi ya Uganda katika maeneo ambayo Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametokea.

Madereva 53 ndiyo wanaingia katika mbio za mchujo baada ya kumaliza ukaguzi wa njia siku ya Jumanne na zoezi la ukaguzi wa magari mapema jana.

“Tuko vizuri na tumejiandaa vyema na tuna ari ya kushinda,” alisema Yassin Nasser ambaye ataongozwa na msoma ramani Mganda Ally Katumba ndani ya Ford Fiesta R5.

Licha ya kuchezwa kama raundi ya pili ya mbio za magari ubingwa wa Afrika, mashindano haya ambayo rasmi yanajulikana kama Shell V Power Pearl of Africa Rally, pia ni raundi ya tatu ya ubingwa wa taifa ya Uganda kwa mwaka huu.

Raundi ya pili ya mbio za ubingwa wa Afrika, kwa mujibu wa orodha ya magari, ni vita ya injini kati ya Skoda Fabia na Ford Fiesta kwa upande wa gari za daraja ya juu, wakati kwa daraja la kawaida, ni mchuano kati ya Mitsubishi Evolution na Subaru Impreza.

Vita ya Skoda na Ford itaanzishwa na Karan Patel wa Kenya ambaye gari yake Skoda Fabia ambaye ataondoka ya kwanza na kufuatiwa na Mtanzania Yassin Nasser atakayekuwa nyuma ya usukuani wa Ford Fiesta R5.

Bingwa mwingine kutoka Kenya, Samman Vohra, na msoma ramani wake Drew Sturrock ataondoka wa tatu akiwa pia na Skoda Fabia.

Mashindano haya ambayo yanaanza rasmi leo, yanategemewa kutamatika siku ya Jumapili, Mei 11 mwaka huu ambapo mshindi atajulikana.

Mtanzania mwingine, Prince Charles Nyerere ataondoka wa 10 akiendesha gari aina ya Mitsubishi Evolution X. Eneo la Rukaari Resort ndiyo mahala ambapo mbio maalum za mchekecho (shakedown) zinaanza asubuhi hii, kwa mujibu wa waandaaji, Shirikisho la Mbio za Magari nchini Uganda(FMU).

Raundi mbili za mwisho, zitapigwa siku za Jumamosi na Jumapili.