Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tano za Yanga zaitisha Ihefu

UBORA wa kikosi cha Yanga na hasa ile dozi ya 5G iliyogawa kwenye mechi tatu mfululizo zikiwamo mbili za Ligi Kuu na moja ya Ligi ya Mabingwa Afrika, imemfanya kocha wa Ihefu Zuber Katwila kujipanga zaidi ili kuwakabili watetezi hao katika mchezo ujao wa ligi utakaopigwa kwenye Uwanja wa Highland Estate, Mbeya.

Yanga itakuwa wageni wa Ihefu mechi itakayopigwa Oktoba 4 huku ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwenye Uwanja wa Highland na kutibuliwa rekodi ya kucheza mechi 49 mfululizo bila kupoteza msimu uliopita, huku Ihefu ikianza hovyo msimu huu ikishinda moja na kupoteza mbili ikiwamo ya nyumbani.

Katwila aliliambia Mwanaspoti kuwa, Yanga ni kati ya timu bora ikiwa pia ni watetezi wa Ligi Kuu, hivyo ni lazima ijipange na itakapokuwa nao iwe makini isitiwe aibu kama JKT na KMC zilizopigwa 5-0 kila moja.

“Msimu uliopita tuliwafunga na kuwatibulia rekodi yao, hayo yashapita hatuwezi kulinganisha mchezo ule na huu, kikubwa tunatakiwa kupambana kupata pointi tatu na sio kukaza kuwafunga,” alisema nyota huyo wa zamani wa kimataifa aliyekipiga Mtibwa Sugar na Taifa Stars na kuongeza;

“Tunaiwekea mikakati kiufundi na ukiangalia msimu huu ni mechi ya yetu ya nne tofauti na uliopita ilikuwa ya mwishoni hivyo itakuwa mechi ya tofauti,” alisema.