Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanga, Moro zang’ara UMITASHUMTA

UMITASHUMTA Pict
UMITASHUMTA Pict

Muktasari:

  • Moro iliishinda Dodoma kwa mikimbio 54, huku Tanga ikishinda  dhiddi ya Dar es Salaam..

TIMU za Morogoro na Tanga zimeanza kwa moto michuano ya Michezo ya Shule za Msingi nchini (UMITASHUMTA) inayoendelea mkoani Iringa kwa kuzisambaratisha Dodoma na Dar es Salaam mtawalia.

Moro iliishinda Dodoma kwa mikimbio 54, huku Tanga ikishinda  dhiddi ya Dar es Salaam..

Mchezo wa Kriketi unaingia kwa mara ya kwanza katika michezo ya UMITASHUMTA baada ya jitihada kubwa za Chama Cha Kriketi nchini (TCA) .

Katika mechi hiyo ya mizunguko 20, Wasichana wa Morogoro ndiyo waliopata kura ya kuanza kubeti na kwa ustadi mkubwa, walitengeneza mikimbio 117 huku wakipoteza wiketi mbili.

Dodoma ilijitutumia na kujikuta wakigota kwenye mikimbio 63 huku wakiangusha wiketi tisa na kupoteza kwa mikimbio 54.

Wasichana wa Tanga ilishinda wiketi tisa dhidi ya Dar es Salaam katika mechi ya UMITASHUMTA inayoendelea mkoani Iringa.

Dar es Salaam ndiyo iliyoanza kubeti na kutengeneza mikimbio 43 baada ya wote 10 kutolewa wakiwa wametumia mizunguko 13 kati ya 20  ya mchezo huo.

Wakitumia mizunguko minne kati ya 20, Tanga ilipiga mikimbio 44 na kushinda mechi huku wakipoteza wiketi moja.

Tanga pia ilikuwa bora kuliko Dar esa Salaam kwa upande wa wavulana na iliifunga wiketi tisa katika mchezo mkali wa kusisimua.