Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Straika Mtanzania apitia haya Zambia

STRAIKA Pict
STRAIKA Pict

Muktasari:

  • Trident Queens alisaini mkataba wa mwaka mmoja akitokea Tanzania ambako alikuwa anahudumu nafasi ya msemaji wa Mlandizi iliyoshuka daraja.

ALIYEWAHI kuwa Ofisa Habari wa Mlandizi Queens, Sajda Sadick ambaye kwa sasa anakipiga Trident Queens ya Zambia amesema licha ya changamoto alizopitia nchini humo za kunyimwa pasi bado alisimama imara.

Trident Queens alisaini mkataba wa mwaka mmoja akitokea Tanzania ambako alikuwa anahudumu nafasi ya msemaji wa Mlandizi iliyoshuka daraja.

Akizungumza na Mwanaspoti, Sajda alisema ilifikia kipindi kocha aliona wazi wachezaji wenzie hawampi pasi ilihali yeye ni mshambuliaji.

Aliongeza mambo yalikuwa magumu zaidi baada ya kocha huyo kuondolewa na kuletwa mwingine ambaye naye aliamini uwezo wake lakini changamoto ilikuwa kwa viongozi.

“Huku changamoto sana, timu za Zambia hawajazoea kuwa na wachezaji wa kigeni, wakati najiunga na timu nilikubalika na nikasaini mkataba, kocha akafukuzwa lakini benchi la ufundi lilikuwepo.

“Niliangaliwa kwenye mechi tano za mwisho ambazo nilikuta zimesalia, sijacheza mechi 14 na nilifanya mazoezi tu na timu lakini bado ilikuwa changamoto, nashukuru nilipambana sikukata tamaa.”

Mkataba wake na timu hiyo unaisha msimu huu na kuhusu ataendelea kikosini hapo au ametafuta timu sehemu nyingine na hapa anajibu.

“Ofa zipo nyingi nje na Zambia naamini sitaendendelea, unajua Mungu hamtupi mja wake, wakati nacheza mechi za kirafiki kuna timu zilikuwa zinafuatilia, kwa hiyo tumeshamaliza taratibu zote na naenda kujiunga nao kuanza Pre Season.”