Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Taifa Stars mpaka raha

Mrisho Ngassa (kushoto)akiwania mpira na mchezaji wa Malawi wakati wa mchezo kati ya   Taifa Stars dhidi ya  Malawi uliofanyika jana .

Muktasari:

Chini ya Kocha Mkuu mzawa, Boniface Mkwasa, Stars ilifanya kweli kwa kuilaza Malawi mabao 2-0 katika pambano kali na tamu lililochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

MNATAKA nini? Tunataka Bao. Mnataka Nini? Tunataka bao.

Ndivyo Taifa Stars ilivyowapa raha Watanzania jana Jumatano baada ya kupata ushindi muhimu nyumbani dhidi ya The Flames ya Malawi katika mchezo wa kwanza wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018.

Chini ya Kocha Mkuu mzawa, Boniface Mkwasa, Stars ilifanya kweli kwa kuilaza Malawi mabao 2-0 katika pambano kali na tamu lililochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Malawi iliyoundwa na wachezaji vijana, ilionekana kuibana Stars dakika 15 za awali kabla ya Mbwana Samatta kuiandikia Tanzania bao la kuongoza katika dakika ya 18 akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Thomas Ulimwengu.

Wakati Malawi ikijiuliza namna ya kurejesha bao hilo, uzembe uliofanywa na kipa Simplex Nthala katika kudaka shuti la krosi ya Haji Mwinyi, uliiwezesha Stars kupata bao la pili katika dakika ya 22 baada ya Ulimwengu kuumalizia mpira uliomgonga kipa huyo.

Katika mchezo huo uliochezeshwa vema na mwamuzi, Hagi Yabarow Wiish, kutoka Somalia, Malawi ilifanya mashambulizi makali ya kushtukiza na kama si umakini wa safu ya ulinzi ya Stars chini ya kipa Ally Mustafa ‘Barthez’, hadithi ingekuwa nyingine.

Stars inaweza kujilaumu kwa kushindwa kuibuka na ushindi mnono kutokana na kukosa mabao mengi ya wazi, ingawa mashabiki walionyesha kufurahishwa na ushindi huo wa nyumbani wakiamini inaweza kwenda kuing’oa Malawi nyumbani kwao siku ya Jumapili.

Iwapo Stars itaing’oa Malawi katika mchezo huo wa marudiano, itafuzu raundi ya pili ya michuano hiyo kwa kukutana na vinara wa soka wa sasa wa Afrika, Algeria katika mechi zitakazochezwa mwezi ujao kati ya Novemba 9 hadi 17.

Vikosi vya jana vilipangwa hivi;

Tanzania; Ally Mustafa ‘Barthez’, Shomary Kapombe, Haji Mwinyi, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani, Himid Mao, Thomas Ulimwengu, Said Ndemla, Mrisho Ngassa/Salum Telela, Thomas Ulimwengu/Ibrahim Ajibu na Farid Mussa/Simon Msuva.

Malawi: Simplex Nthala, Stanley Sanudi, Mivale Gabeya, Yamkani Fadya, Limbikani Mzava, Gerard Phiri, Chimango Kayira, Micium Mhone/Mamase Chiyasa, Chawangiwa Kawanda, John Banda/Gabadinho Mhango na Robin Ngalande.

Katika michezo mingine ya jana, Comoro na Lesotho zilitoka sare ya 0-0, Burundi ikishinda ugenini bao 1-0 dhidi ya Shelesheli wakati mchezo wa Sudan Kusini na Mauritania ulivunjwa na mvua kubwa kipindi cha kwanza huku timu zikiwa 1-1.