Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yamaliza kikao na TPLB, yashikilia 'hatuchezi'

Muktasari:

  • Mkutano huo ambao ulianza saa 4:30 na kumalizika saa 6:53 mchana ukifanyika kwenye ofisi za bodi hiyo zilizopo Ilala jijini Dar es Salaam.

Mkutano wa Bodi ya Ligi Tanzania TPLB na viongozi wa  Yanga umemalizika na makamu wa rais wa klabu hiyo ametoa neno kilichojiri ndani.

Mkutano huo ambao ulianza saa 4:30 na kumalizika saa 6:53 mchana ukifanyika kwenye ofisi za bodi hiyo zilizopo Ilala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya mkutano huo Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji, amesema klabu yao imeshiriki kikao hicho kuwasilisha msimamo wa wanachama na mashabiki wao.

Akizungumzia kuhusu mustakabali wa mchezo huo dhidi ya Simba, Arafat amesema Yanga haikuwahi kusema kama itacheza mechi hiyo.

"Tumemaliza mkutano na tulichofanya ni kuwasilisha msimamo wa klabu kutoka kwa wanachama na mashabiki wetu hilo ndio kubwa,"amesema Arafat.

Mara baada ya mujibu swali hilo Arafat aliondoka eneo hilo sambamba na viongozi wenzake.

Afisa Habari wa Bodi ya Ligi Karim Boimanda amesema taarifa kamili juu ya mkutano huo itatolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi Almas Kasongo.

Awali kabla ya taarifa hiyo, Yanga kupitia kwenye kurasa zao za kijamii ilisema kuwa viongozi wake walikaa kwenye kikao cha saa kadhaa na viongozi wa bodi na kuwasilisha msimamo wa klabu kuwa hawatashiriki mchezo wa Juni 15, 2025 hadi matakwa yao waliyowasilisha Bodi ya Ligi kwa maandishi yatakapotekelezwa.

Mechi hii awali ilipangwa kupigwa Machi 8, 2025 lakini siku moja kabla Simba iliandika barua ya kulalamika kuwa imezuiwa kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Mkapa sehemu ambayo ndiyo mchezo huo ulikuwa unafanyika na wale wanaodaiwa kuwa walinzi wa Yanga.

Saa chache kabla ya mchezo huo, Bodi ya Ligi ilitoa taarifa ya kuahirisha mechi hiyo, jambo ambalo liliwaudhi Yanga na kutangaza kuwa hawatacheza mchezo mwingine hadi watakapopewa taarifa rasmi kwanini mechi ya kwanza haikufanyika.