TAFF kuja na kituo cha soka kwa watu wenye ulemavu

SHIRIKISHO la soka kwa watu wenye Ulemavu nchini Tanzania(TAFF) linatarajia kufungua kituo cha kutafuta na kukuza vipaji vya soka kwa watu wenye ulemavu.
Amelithibitisha hilo Rais wa Shirikisho hilo, Peter Sarungi na kusema kuwa wao kama Shirikisho wameona kuwa Kuna umuhimu mkubwa wa kufungua kituo maalumu ambacho kitakua na jukumu la kuvikuza vipaji vya soka hapa nchini hususani kwa watu wenye ulemavu.
"Tunatarajia kukifungua kituo hicho hivi karibuni mara baada ya timu ya taifa 'Tembo warriors' kurejea kambini kwaajili ya kujiandaa na kombe la Duniani" aliendelea na kusema kuwa;
"Tumeona Kuna sababu kubwa ya kufungua kituo hicho kwani tumeona huitaji mkubwa wa walemavu wanasakata kandanda kutaka kituo hicho" alisema Sarungi.
Aidha pia kwa upande wa katibu wa Shirikisho hilo, Mosses Mabulla alisema kuwa huu ni wakati wa wadau wa soka Nchini kuwekeza kwenye soka la walemavu.
"Tunawakaribisha wadau wa soka nchini kuanza kuwekeza kwenye soka la walemavu kwani kupitia uwekezaji wao basi tunaweza kufanya makubwa na kulitangaza Taifa kupitia mchezo huu" alisema Mabulla.
Timu ya taifa ya walemavu Tembo Warriors inatarajiwa kuingia kambini mwezi wa pili mwanzoni ambapo pia inasemwa kuwa huenda wakaenda kuweka kambi mkoani Arusha.