Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tabora United mdaka mishale kutoka Gabon

Muktasari:

  • Tabora United inaendelea kujiimarisha maeneo mbalimbali ikiwemo golini kufuatia kuondoka kwa Hussein Masalanga aliyerejea Singida Black Stars baada ya kuitumikia timu hiyo kwa mkopo huku Victor Sochima akiondolewa.

MUDA wowote Tabora United inaweza kumtangaza kipa raia wa Gabon, Jean Noel Amonome baada ya kukamilika ishu ya makubaliano ya mkataba.

Tabora United inaendelea kujiimarisha maeneo mbalimbali ikiwemo golini kufuatia kuondoka kwa Hussein Masalanga aliyerejea Singida Black Stars baada ya kuitumikia timu hiyo kwa mkopo huku Victor Sochima akiondolewa.

Katika kuimarisha eneo hilo, Tabora United imemchukua Fikirini Bakari kwa mkopo akitokea Singida Black Stars na sasa imemuongeza Amonome.

Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo zinadai kuwa Amonome anayetokea AS Arta Solar ya Djibouti, tayari ametua nchini kwa ajili ya kujiunga na kikosi hicho chenye maskani yake mjini Tabora.

Chanzo cha taarifa kimesemakuwa baada ya mazungumzo kukamilika, kipa huyo mwenye umri wa miaka 27 amekubali kusaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwingine.

“Tayari mchezaji huyo ameshawasili hapa nchini kuja kumalizia mambo madogo yaliyobaki kabla ya kuanza kuitumikia timu. Mambo yanafanyika haraka ukizingatia kwamba dirisha la usajili linaelekea kufungwa,” kilisema chanzo chetu cha taarifa.

Kocha wa Tabora United, Anicet Kiazayidi kutoka DR Congo wakati usajili wa dirisha dogo ukifunguliwa Desemba 15, 2024, aliwasilisha ripoti ya maeneo yanayohitaji kufanyiwa marekebisho ikiwemo nafasi ya kipa ambayo imefanyiwa kazi na viongozi wa klabu hiyo.