TAARIFA KWA UMMA
Tunasikitika kuwaarifu wasomaji wetu wapendwa kuwa tunalazimika kusitisha uchapishaji wa maudhui mtandaoni kuanzia sasa kufuatia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kusitisha leseni zetu za utoaji wa huduma ya maudhui mtandaoni kwa siku 30 kutokana na kuchapisha maudhui yaliyozuiwa yanayokiuka Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni za 2020.
Mwananchi Communications Limited (MCL) inaahidi kuwaletea wateja na wasomaji wetu habari, taarifa na maudhui bora yanayowezesha taifa kupitia magazeti yetu, na huduma zetu nyingine zisizo za mtandaoni wakati tukiendelea kuzungumza na mamlaka husika ili kupata muafaka. Tunawashukuru sana kwa kuendelea kuwa nasi.
Imetolewa na
Victor A. Mushi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Mhariri Mtendaji Mkuu
Mpoki Thomson Mhariri Mkuu Mtendaji Msaidizi na Mhariri Mtendaji, The Citizen