Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Suarez ametoka kwa rafiki anaenda kwa rafiki mwingine

 ALAN Dershowitz. Mwanasheria nguli wa Marekani. Kiburi anayejiamini. Aliwahi kusema, “Mimi ni mtu mgumu na napambana sana na sikati tamaa. Na hilo huwa linanipatia marafiki na maadui. Najua hilo.”

Inachekesha sio. Alisema kweli. Nimemkumbuka Dershowitz majuzi wakati nilipomuona Luis Suarez akitoa machozi mbele ya mkutano na waandishi wa habari pale Camp Nou. Inahuzunisha kusema kwaheri kwa marafiki wa karibu. Inahuzunisha kuipa mgongo wa kwaheri moja kati ya klabu kubwa duniani.

Inahuzunisha kuachana na Lionel Messi. Rafiki yake wa karibu zaidi katika soka. Inakwenda katika pande mbili. Hata Messi huyu Suarez anabakia kuwa rafiki yake wa karibu zaidi katika soka. Zamani tulidhani ni Sergio ‘Kun’ Aguero, lakini sasa tumegundua Suarez ni rafiki zaidi wa Messi.

Urafiki wao ulianzia 2014 wakati Suarez alipomng’ata beki wa Italia, Giorgio Chiellini katika pambano la Kombe la Dunia kati ya Uruguay na Italia, kisha akaamua kuhamia Barcelona. Akatengeneza urafiki mkubwa na Messi. Sijui kwa sababu wote wanatoka Amerika Kusini. Hatujui. Hadi familia zao ni marafiki waliopitiliza.

Suarez anaachana na Messi na Barcelona. Sasa anakwenda kwa rafiki mwingine wa kweli zaidi. Huyu rafiki amepatikana kutokana na kile ambacho Dershowitz amewahi kutuambia. Amepatikana kutokana na tabia zake kuwa mtu mgumu.Hesabu wachezaji wagumu waliobaki katika soka. Wapo wachache. Miongoni mwao wanabakia kuwa kama Suarez mwenyewe, Diego Costa, nani mwingine? Unaweza kuwakumbuka. Hawa ndio watu ambao Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone anawataka. Tabia hii ya ugumu imemzalishia Suarez maadui wengi kama ambavyo mashabiki wengi wanamuona adui. Tangu alipomng’ata Branislav Ivanovic katika pambano la Liverpool na Chelsea na kisha alipomng’ata Chiellini.

Lakini pia tabia hii ya ugumu imempatia marafiki kadhaa. Mimi ni mmoja wao lakini rafiki mwingine aliyemtengeza ni Diego Simeone. Hawa ndio watu ambao Simeone anawapenda. Wapiganaji. Wanaotoa kila kitu hata kung’ata kwa ajili ya kushinda pambano la soka.

Niliposikia Simeone anamtaka Suarez sikupata shida kujua kinachoongelewa ni kweli au hapana. Simeone anapenda wachezaji wa Suarez kwa sababu na yeye ana tabia hizihizi za Suarez. Mtu mmoja aliwahi kusema: “Nionyeshe marafiki zako nitakwamba wewe ni nani”. Mwingine naye akaongeza kwa kusema: “Ukitaka kujua tabia ya Jenerali watazame mabrigedia wake??. Sijui kama kuna yeyote alikosea kati yao. Simeone amemruhusu, Alvaro Morata kwenda Juventus na sijashangaa kwa sababu Morata ni laini. Hawezi mikikimikiki kama ile ambayo Suarez au Costa wanaweza kukupa katika eneo la mwisho. Hawa ndio mabrigedia wake halisi.

Kitu ambacho kimewahi kunishangaza katika uhamisho wa soka ni pale kinda, Joao Felix, alipohamia Atletico Madrid. Nilijua anajirudisha nyuma katika maendeleo ya soka. Joao ni kinda mwenye kipaji kikubwa, lakini hawezi kuendelea katika staili ya soka la Simeone.

Joao anahitaji timu ambayo itashambulia. Timu ambayo itacheza soka maridadi ili aonyeshe kipaji maridhawa. Joao hapaswi kuchezea timu ambayo inaridhika na ushindi wa bao 1-0, kisha inaanza kucheza soka la kujihami na kufanya mashambulizi machache ya kushtukiza.

Kwa Suarez, Simeone atakuwa amempata punda ambaye yuko tayari kuachwa mbele peke yake akipambana huku timu ikiwa mita chache kutoka alipo. Na kama tunavyomjua Suarez anaijua kazi hii. Atapiga ‘tackling’, atacheza rafu, atagombana na walinzi wa timu pinzani, mwishowe anaweza kung’ata pia. Usimuamini sana.

Kitu kinachonifurahisha ni kufikiria kama Suarez na Costa wanaweza kucheza pamoja. Nadhani Costa anaweza kuondoka Atletico lakini kama akibaki basi itachekesha kidogo kuona wanyama wawili wabaya wakiongoza safu ya ushambuliaji ya Simeone. Kocha pekee ambaye atakuwa anajuta kutowahi kufanya kazi na Suarez ni Jose Mourinho. Aliwahi kufanya kazi na Costa, lakini nadhani angetamani zaidi kufanya kazi pia na Suarez. Hawa ndio aina ya wachezaji wake. Wanyama.

Kitu kingine ambacho kimenichekesha zaidi ni pale niliposikia Simeone anamtaka sana kiungo wa Arsenal, Lucas Torreira. Hawa pia ni aina ya wachezaji wake. Torreira ni mfupi kwa kimo, lakini ni mnyama kama Suarez. Torreira hatasimama uwanjani. Atakaba hadi kivuli. Sijui kwanini ameshindwa kung’ara Arsenal chini ya Mikel Arteta, lakini nadhani Arteta anahitaji wachezaji wenye akili zaidi ya mpira kuliko simba wapambanaji. Nini hatima ya Suarez? Nadhani anaelekea ukingoni. Umri haumruhusu kurudia makali yake ya Liverpool au ya Barcelona.

Wakati ukuta. Lakini ana mwaka mmoja au miwili ya kuipatia kitu Atletico Madrid na mashabiki watampenda. Barcelona? Sina shaka na uamuzi wa Ronald Koeman. Huu ulikuwa ni wakati sahihi wa kuachana na Suarez na kujenga kikosi upya kama anavyotaka.

Mtu ambaye hauwezi kuachana naye kwa sasa ni Messi ambaye hata akicheza asilimia 40 tu ya uwezo wake anakuwa hatari kuliko Bukayo Sana wa Arsenal. Kwa Suarez ungeweza kuona ameachwa nyuma kidogo na baadhi ya washambuliaji bora duniani tofauti na miaka michache iliyopita. Majeraha yamemuweka kando kwa vipindi virefu tofauti lakini pia umri unamtupa mkono.

Suarez wa leo hawezi kulinganishwa na Pierre- Emerick Aubameyang au Roberto Lewandowski.