Stars wamebana, wameachia

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

MCHEZO wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kati ya Guinea ya Ikweta na Tanzania ‘Taifa Stars’ umemalizika kwa wenyeji Guinea kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

MCHEZO wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kati ya Guinea ya Ikweta na Tanzania ‘Taifa Stars’ umemalizika kwa wenyeji Guinea kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Matokeo hayo yanaifanya Taifa Stars kupoteza matumaini ya kufuzu kucheza Afcon mwakani kutokana na kuwa na alama chache huku Guinea ya Ikweta wakisonga mbele.

Mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Nuevo Estadio de Malabo ulikuwa wenye presha kubwa kwa wachezaji wa Stars kutokana na ubora wa Guinea ya Ikweta.

Licha ya kwamba Guinea walionekana muda mwingi kulishambulia lango la Stars lakini wachezaji wa kikosi hicho hususani eneo la kiungo na mabeki wa Stars walijitahidi kuzuia mashambulizi hayo wakiongozwa na Aishi Manula aliyesimama imara langoni akiokoa michomo kibao.

Yote hayo hayakuwazuia Guinea kuchoka kulishambulia lango la Stars na dakika ya 89 walipata bao la kuongoza na la ushindi kupitia kwa Emilio Nsue aliyefunga akiwa katikati ya msitu wa mabeki wa Stars na kupiga kiki kali iliyomshinda kudaka kipa wa Stars na kuzama Wavuni.

Baada ya matokeo hayo Guinea ya Ikweta wanafikisha alama tisa wakiungana na Tunisia wenye alama 13 kutoka kundi hilo (J) kufuzu kushiriki Afcon mwakani nchini Cameroon.

Kwa maantiki hiyo, matokeo ya mechi za duru ya mwisho kwa kundi hilo hayatabadili msimamo wa kundi hilo ambapo tayari Libya na Stars wamekosa nafasi ya kushiriki michuano hiyo mwakani.

Matokeo mengine kutoka kwenye kundi hilo Tunisia amempiga bao 2-1 Libya na kufuzu moja kwa moja.