Stars kundi E kufuzu Kombe la Dunia

Muktasari:
- Stars imepangwa kundi E ikiwa pamoja na timu sita ambazo ni Morocco ambayo ilifika nusu fainali Kombe la Dunia 2022, Zambia, Congo, Niger na Eritrea
Droo ya makundi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 imechezeshwa leo saa 1 usiku jijini Abidjan, Ivory Coast, .
Stars imepangwa kundi E ikiwa pamoja na timu sita ambazo ni Morocco ambayo ilifika nusu fainali Kombe la Dunia 2022, Zambia, Congo, Niger na Eritrea
Kundi A zimepangwa timu kama Egypt, Bukina Faso, Guinea Bissau, Sierra Leone, Ethiopia na Djibout huku kundi B ambalo linaongozwa na Senegal ‘ Simba wa Teranga’, DR Congo, Mauritania, Togo, Sudan, Sudani ya Kusini
Kundi C ambalo limeanza Nigeria, Afrika ya Kusini, Benin, Zimbabwe, Rwanda na Lesotho ambapo kundi linalofuatia ni D kuna Cameroon, Cape Verde, Angola, Libya, Eswatini na Mauritius.
Timu ya Taifa Stars ndo inafuata ambapo ipo kundi E likifuatiwa na kundi F ambalo linatimu sita kama makundi mengine inatimu kama Cote D’ivoire, Gabon, Kenya, The Gambia, Burundi na Seychelles
Makundi matatu ya mwisho ambalo ni kundi G linaongozwa na Algeria, Guinea, Uganda, Mozambique, Bostwana na Somalia, kundi H ni Tunisia, Equatorial Guinea, Namibia, Malawi, Liberia na Sao tome & Principe na mwisho ni kundi I ambalo lina timu kama Mali, Ghana, Madagascar, Cetral African, Comoros na Chad