Stars hali ngumu kwa Mkapa

Tuesday January 12 2021
stars 2 pic
By Thomas Ng'itu

MORALI ya wachezaji wa kikosi cha Tanzania 'Taifa Stars' ilionekana kuwa ndogo katika dakika 45 za kipindi hali ambayo iliwafanya wapinzani wao DR Congo kutawala mchezo.

Namna ambavyo Stars walikuwa wanacheza ni kama vile hawapo nyumbani, kwani DR Congo waliweza kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa na kushambulia mara kwa mara.

Dakika 8 Masasi Amede alifyatuka shuti kali je ya boksi na mpira kutoka pembeni kidogo ya goli na kufanya mashabiki wapige shangwe.

Ndani ya dakika 15 za kipindi cha kwanza, Stars walionekana kuzidiwa mipango na DR Congo kiasi cha kunyimwa uhuru wa kucheza.

DR Congo walikuwa wanawalazimisha Stars kucheza katika upande wao hali ambayo iliwafanya wachezaji wa Congo kuwashambulia mara kwa mara.

Dakika 19 DR Congo walipata bao la kwanza baada ya Mayele Kalala kupiga mpira wa chinichini ambao kipa wa Stars, Juma Kaseja alishindwa kuudaka baada ya kuteleza na mpira kwenda wavuni.

Advertisement

Uwezo wa kumiliki mpira kwa wachezaji wa DR Congo ulionekana kuwa mkubwa tofauti na kwa upande wa Stars.

Dakika 43 kiungo wa DR Congo, Kinzumbi Philipe alimchungulia kipa wa Stars, Juma Kaseja kwa kupiga mpira wa kukevu lakini ulipanguliwa na kuwa kona isiyokuwa na faida.

Dakika 45 DR Congo walitaka kupata bao la pili kupitia kwa Mayele Kalala ambaye alimtoka vizuri kipa Juma Kaseja wote wakiwa nje ya boksi na mchezaji huyo kupiga mrefu na kuzuiwa na beki Carlos Protas.

KIUNGO CHAKATIKA

Katika dakika 45 za kipindi cha kwanza viungo wa Stars hawakuwa bora katika kutengeneza mipango ya kutafuta bao.

Hali hiyo iliwalazimu kutumia nguvu katika kukaba kuliko kutengeneza nafasi ya kufunga ili wasiweze kuruhusu bao kwani viungo wa DR Congo walikuwa bora.

Kocha Ndayiragije aliwapanga Said Ndemla, Feisal Salum na Lucas Kikoti katika eneo hilo lakini walionekana kutoendana na kasi ya DR Congo ambao walikuwa wepesi katika kuwapokonya mipira na kusambaza.


Kikosi Stars:Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Yassin Mustapha, Ibrahim Ame, Aggrey Morris, Said Hamisi, Ayoub Lyanga, Feisal Salum, Adam Adam, Lucas Kikoti na Deus Kaseke.

Kikosim DR Congo: Matampi Ngumbi, Issama Mpeko, Luzolo Nsita, Inomga Baka, Idumba Fasika, Masasi Amede, Kinzumbi Philipe, Mika Miche, Mayele Kalala, Kimvudi Kiekie na Lilepo Makabi.

Advertisement