Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Srelio yainyoosha Mgulani JKT

SCERIO Pict

Muktasari:

  • Tambo za kocha huyo zimekuja baada ya kuwepo na muunganiko mzuri wa wachezaji wake kwa sasa, tofauti ilivyokuwa katika michezo yao ya mwanzo.

BAADA ya Srelio kuifunga Mgulani JKT kwa pointi 107-64, kocha wa timu hiyo Miyasi Nyamoko amesema ushindi huo umewanyooshea njia ya kucheza hatua ya nane bora.

Tambo za kocha huyo zimekuja baada ya kuwepo na muunganiko mzuri wa wachezaji wake kwa sasa, tofauti ilivyokuwa katika michezo yao ya mwanzo.

“Timu ilikuwa inabezwa na kila mtu lakini tutakuja kuwashangaza na watakuja kutufahamu ligi itakapomalizika,” alitamba Nyamoko.

Katika mchezo huo, Srelio iliongoza robo zote nne kwa pointi 30-9, 27-20, 28-16 na 22-4.

Mchezaji Junior Louissi wa Srelio alifunga pointi 30, akifuatiwa na Mussa Mwakalobo aliyefunga pointi 15.

Louisisi ambaye ni raia wa Gabon aliongoza kwa kudaka mipira ya rebound mara 13.

Kwa upande wa Mgulani JKT, Yassini Shabani alifunga pointi 40, huku akifunga eneo la mtupo mmoja 'three pointi' 21, akifuatiwa Dotto Zephanie  aliyefunga 10.

Srelio ilianza ligi hiyo kwa kufungwa na Mchenga Star kwa pointi 82- 70, Dar City pointi 105-32, DB Oratory pointi 76-72, baadaye ikaifunga Chui pointi 55-52 na Mgulani JKT pointi 107-64.

Ligi hiyo, itaendelea leo kwa mchezo kati ya Twalipo Queens na Tausi Royals, Polisi Stars na Jeshi Stars, huku upande wa wanaume DB Oratory itaumana na Outsiders na Polisi itacheza dhidi ya ABC.