Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yatema wawili!

Muktasari:

SIMBA wameachana na wachezaji wake wawili straika, Mnigeria Junior Lokosa na beki Mzimbabwe Peter Muduhwa ambao wote walisajiliwa katika dirisha dogo.

SIMBA wameachana na wachezaji wake wawili straika, Mnigeria Junior Lokosa na beki Mzimbabwe Peter Muduhwa ambao wote walisajiliwa katika dirisha dogo.

Wachezaji hao walisajiliwa katika dirisha dogo la shirikisho la soka Afrika (CAF), kwa ajili ya kwenda kuongeza nguvu katika Ligi ya mabingwa Afrika ambayo wapo hatua ya robo fainali.

Mwanaspoti limepata habari za uhakika kutoka ndani ya Simba kuwa Muduhwa na Lokosa usajili wao hapakuwa na (Sign feels), ila walikuwa wanavuta mishahara minono.

Muduhwa na Lokosa walisajiliwa kwa mkataba wa miezi sita kianzia Januari waliposajiliwa mpaka, Juni lakini mikataba yao ilisitishwa ndani ya miezi minne tu.

Nyota hao kila mmoja ikifika mwisho wa mwezi alikuwa anavita Dola za Kimarekani 5000 ambayo kwa pesa ya Kitanzania ni zaidi ya Sh11 milioni.

Kwa maana hiyo kila mmoja amevuta si chini ya Sh44 milioni kwa muda wa miezi minne aliyokuwa katika kikosi hicho kwa maana hiyo wawili hao wamechukua Sh88 milioni kama mishahara kwa muda waliokuwa hapo.

Pesa hiyo ya mshahara ambayo wamechukua wachezaji hao wawili mbali na zile bonansi ambazo zinatolewa kila timu hiyo inaposhinda mechi ya kimataifa.

Wachezaji hao licha ya kuchukua pesa hizo ndefu hawakupata nafasi ya kucheza mechi yoyote ya kimashindano wala kuwa katika benchi la wachezaji wa akiba.

Muduhwa alikuwa anashindwa kucheza nafasi yake kwani Joash Onyango na Pascal Wawa ndio walikuwa wanacheza mara kwa mara lakini mbadala wao alikuwa Kennedy Juma na Ibrahim Ame.

Wakati Lokosa alicheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya TP Mazembe ambayo aliingia kipindi cha pili hakucheza kimataifa hakuwa fiti na nafasi yake wanatumika mara kwa mara, Chriss Mugalu, Meddie Kagere na John Bocco.

Baada ya kuachana na wachezaji hao kocha wa Simba, Didier Gomes alisema alikuwa anavutiwa zaidi na Muduhwa ila alikuwa anashindwa kumtumia kutokana hakuwa na ufiti wa mechi.

"Ilikuwa ngumu kumuweka nje Onyango na Wawa ambao walikuwa wanacheza pamoja hata katika Ligi Kuu Bara na kumpanga Muduhwa ingawa ni mchezaji mzuri," alisema Gomes na kuongezea;

"Lokosa mpaka nafika katika kikosi cha Simba hakuwa fiti na alihitaji muda zaidi wa kuandaliwa hali ambayo ingekuwa ngumu kutokana mechi za mashindano zilikuwa zikiendelea."