Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yamganda Pogba wa Zenji

POGBA Pict

WATANI wa jadi wa soka nchini, Simba na Yanga wameendelea ushindani wao nje ya uwanjani kwa kuamua kuvamia visiwani Zanzibar na hususani katika klabu ya Mlandege kwa ajili ya kubeba viungo wanaojua kutembeza boli kwa ajili ya kusuka vikosi vyao kwa msimu ujao wa mashindano.


Ilianza Yanga kwa kuvamia Mlandege na kukamilisha dili la kumnasa kiungo Abdulnassir Mohammed Abdallah 'Casemiro', lakini hilo ni kama limeiamsha Simba ambao nao waliamua kuvuka Bahari ya Hindi hadi visiwani kwa lengo la kumbeba fundi mwingine wa mabingwa hao wa Ligi Kuu Zanzibar.


Ipo hivi. Inaelezwa kuwa Simba nao wameamua kuvamia Zenji kwa kuanza mazungumo na fundi mwingine wa boli Seleman Juma Kidawa 'Pogba'.

Simba imeingia vitani na JKT Tanzania, Tabora United na KMC zilizokuwa zikiwinda saini ya kiungo huyo ambaye anamudu kucheza sita, nane na 10.

Chanzo cha kuaminika kutoka Mlandege kimeliambia Mwanaspoti kuwa baada ya kuwa kwenye mchakato wa kumuuza kiungo wao Casemiro wamepokea ofa nyingine nne za kuwindwa kwa kiungo wao mwingine ambaye pia ananamba nzuri kikosini.

"Pogba na Casemiro ni pacha ammbao wanacheza sambamba kikosini ndio nyota ambao wametumika kwenye mechi zote msimu huu uwiano wao wa kucheza pamoja umezaa matunda na kufanya timu yetu kuwa bora na ya ushindani msimu ulioisha," alisema na kuongeza;

"Baada ya mazungumzo na Yanga kuhusu Casemoro sasa vita mpya ipo kwa Pogba ambaye timu nne kutoka bara zinawania saini yake bado tunaendelea na mazungumzo hatutajua atacheza wapi hadi sasa;

"Mazungumzo na Simba bado hayajaisha lakini wasimamizi wa mchezaji wanaangalia na timu nyingine pia ambazo zimeonyesha nia ya kumuhitaji, muda sio mrefu tutafikia uamuzi wa kati ya hizo sita nilizokutajia," alisema mtoa taarifa huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Mwanaspoti lilipata nafasi ya kuzungumza na kiungo huyo ambaye alithibitisha kuwa amepokea taarifa za uwepo wa ofa hizo huku akiweka wazi kuwa bado anamkataba wa miezi sita na waajili wake Mlandege.

"Nimepewa taarifa juu ya ofa hizo lakini sifahamu mazungumzo yanaendaje nimewaachia wasimamizi wangu na klabu yangu kwani bado nina mkataba wa miezi sita na Mlandege."

Pogba ni zao la kituo cha michezo cha FTI kilichopo Afrika Kusini msimu huu ni msimu wake wa pili kuichezea Mlandege ametumika kwa mechi zote 30.


WARITHI WA TSHABALALA

Katika hatua nyingine wakati sintofahamu ikitanda juu ya kumbakiza beki mkongwe mwenye mafanikio makubwa ndani ya Simba, Mohammed Hussein 'Tshabalala', mabosi wa klabu hiyo wameanza kujadili majina ya nyota wawili wanaoweza kuziba pengo la beki huyo wa kushoto.

Tshabalala anayeitumikia timu hiyo kwa zaidi ya miaka 10 hadi sasa bado hajasaini mkataba mpya, lakini mezani kwa Simba kuna majina ya mabeki  wawili, Antony Mligo wa Namungo na Karim Bakir anayekipiga JKT Tanzania.

Wawili hao wanatajwa kupelekewa ofa mezani kwa ajili ya kusaini mikataba ya kuitumikia Simba msimu ujao 2025/26, huku ikielezwa mazungumzo baina ya pande zote mbili yanaendelea.

Mwanaspoti limepenyezewa taarifa kuwa Simba licha ya kutomalizana na Tshabalala, lajkini wameamua kuingia sokoni kusaka saini ya moja kati ya nyota hao ili kuongeza nguvu kikosini mwao.

"Ni kweli Tshabalala hajaongeza mkataba, lakini hilo halizuii sisi kutafuta wachezaji wengine hakuna nafasi ya mchezaji mmoja misimu yote na ndio maana aliongezwa Valentin Nouma," alisema chanzo hicho kutoka Simba na kuongeza;

"Mligo na Bakiri mazungumzo bado yanaendelea mmoja kati yao ambaye mchakato utaenda kama tulivyopanga basi atasajiliwa na atakuwa sehemu ya kikosi msimu ujao;

"Wawili hao wote ni panga pangua vikosi vyao vya kwanza kwenye timu wanazocheza na wameonyesha uwezo mkubwa msimu ulioisha hivyo ni nafasi ya kocha kuchagua nani bora zaidi ili kuupa mwanya uongozi ukamilishe dili."

Bakir amepita Biashara United, Alliance, Kagera Sugar, Mbuni FC na sasa anakipiga JKT Tanzania kwa mara ya pili baada ya awali kuanza kuitumikia timu ya vijana alipotafutwa na Mwanaspoti alisema bado ni mchezaji wa JKT Tanzania kwani anamkataba wa mwaka mmoja na nusu ameitumikia miezi sita tu tangu amejiunga nayo dirisha dogo.

"Mimi ni mchezaji halali wa JKT Tanzania kwa mujibu wa mkataba kama kuna ofa nafikiri mazungumzo ni baina ya timu hiyo na waajiri wangu wa sasa siwezi kuzungumzia kitu chochote nje ya timu niliyopo hapo naomb uzungumze na timu yangu wao ndio watakuwa na majibu sahihi." alisema.