Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yagusa dili la Yanga

Muktasari:

  • Mpaka sasa msimamo wa ligi unavyosomeka, Simba na Yanga ndiyo wawakilishi wa Tanzania Bara kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao huku Singida Black Stars na Azam zikienda Kombe la Shirikisho.

DIRISHA kubwa la usajili wa Ligi Kuu Bara linanukia na Mwanaspoti linafahamu kuna kitu kinaendelea baina ya Simba na Yanga nchini DR Congo.

Mpaka sasa msimamo wa ligi unavyosomeka, Simba na Yanga ndiyo wawakilishi wa Tanzania Bara kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao huku Singida Black Stars na Azam zikienda Kombe la Shirikisho.

Habari za ndani ambazo Mwanaspoti linazo ni kwamba watani wa jadi wanamuwania kiungo wa Union Maniema ya DR Congo, Agee Basiala.

Na kila moja tayari imeshatupa karata yake, na kinachofanyika sasa ni mapambano ya chini kwa chini kila moja ikiweka sawa ‘mitambo’ ili kufunga dili mapema.

Yanga ndio iliyoanza kumfuatilia staa huyo tangu dirisha dogo lililopita na ilikuwa inasubiri tu msimu umalizike ili aje kuwa mbadala wa Stephane Aziz KI ambaye tayari ameshauzwa Wydad Casablanca ya Morocco.


SABABU ZA SIMBA

Simba ilipokea ripoti ya kocha Fadlu Davids ikiwataka mabosi wafanye marekebisho katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la kiungo na mambo yafanyike haraka kabla ya dirisha halijafunguliwa kwani ushindani na ugumu utaongezeka sokoni.

Na hapo ndipo ilipoingia kazini na kuanza na kiungo wa Azam, Feisal Salum ambaye bado kuna jambo linaendelea, lakini inaona kuna ugumu unaweza kutokea kwa vile Yanga ina mkono kwenye vipengele vya mauziano ya staa huyo na Azam.

Lakini, vilevile Feisal ana mkataba wa mwaka mmoja na Azam ambayo inahitaji kumtumia msimu ujao kwenye michuano ya kimataifa, ingawa habari za ndani ni kwamba mchezaji mwenyewe anatamani kuondoka.

Mkanganyiko huo ukaifanya Simba kutazama upande wa pili na kuamua kugonga hodi DR Congo kumnasa kiungo Basiala ambaye Yanga pia ilishamuweka kwenye hesabu zake kitambo. Lakini kati ya wawili hao lolote linaweza kutokea.


ISHU YA YANGA

Yanga iliwahi kumtaka Basiala msimu mmoja uliopita ikivutiwa wakati huo akicheza kama kiungo wa pembeni, lakini baadaye akabadilishiwa nafasi na kuchezeshwa kiungo wa kati mshambuliaji nyuma ya mshambuliaji wa mwisho.

Na ndani ya Maniema ndiko alikotoka Maxi Nzengeli na wakati akiwa hapo, Basiala alichukuliwa kama pacha wake - wote wakiifanya timu hiyo kuwa tishio kabla ya Yanga kumnyakua fundi huyo na sasa inataka kumbeba na mwingine.

Mwanaspoti linafahamu kwamba mabosi wa Yanga na Maniema wana ukaribu mkubwa hivyo huenda ikawa rahisi kufanya biashara hiyo ingawa mwisho wa siku klabu hiyo imekuwa mahiri kwenye mauzo ya wachezaji kwa kuangalia zaidi dau.

Chanzo cha ndani Maniema kimeliambia Mwanaspoti: “Yanga wanamtaka Agee (Basiala) kweli. Wapo kwenye mazungumzo na bado hayajakamilika, lakini unajua wale ni marafiki wakati wowote kitu kutoka kwao kinaweza kumalizika kwa haraka ingawa na Simba nao wana nafasi kubwa.”

Kwa mujibu wa wachambuzi wa soka la DR Congo, Basiala ana nguvu ya kumudu kukimbia eneo kubwa uwanjani kama alivyo Nzengeli na pia anajua kutoa pasi za mwisho na kuchezesha timu, lakini pia ni fundi wa kutupia mipira ya adhabu kama Aziz KI  huku akiwa miongoni mwa wachezaji wanaocheza kikosi cha kwanza ndani ya klabu hiyo maarufu.